November 12, 2012

USALAMA BARABARANI,CHUKUA TAHADHALI

Kwa masikio yangu siku moja, askari wa kikosi cha usalama barabarani alimuuliza mpanda Pikipiki, kwanini unatembea bila Helmet? Jamaa bila hata aibu akamjibu, Samahani AAfande sikujua kama nitakutana na wewe! shit...............................Binafsi niliskitika sana afu nikaondoka! Nilijiuliza maswali mengi sana ikiwa ni pamoja na :-

    1. Unavaa Helmet kwa kumuogopa Askari, au kwa usalama wako?
    2.Unapakia abiria namna hiyo(Mshikaki) umeambiwa hilo ni Lory?
    3.Uwezo wa pikipiki yako ukoje? na hiyo Pikipiki unayopakia namna hiyo ni yako,au umeazima? unaendesha ni ya Boss! je anajua kwamba unapakia mizigo namna hiyo?
Na,wewe abiria uliekubali kupakizwa namna hiyo,sawa Maisha magumu,Usafiri wa shida lakini huoni kama ni hatari?

TAFAKARI,CHUKUA HATUA

No comments:

Post a Comment