November 27, 2012

WALEMAVU WAKIWEZESHWA WANAWEZA

Mkuu wa Mkoa wa Kagera kanali Mstaafu Fabian Massawe akizungumza na walemavu wa Bukoba.
Picha kwa hisani ya :- www.bukobawadau.blogspot.com
Baadhi ya bidhaa zinazotengenezwa na walemavu
Bango linalohamasisha kununua bidhaa zinazotengenezwa na walemavu kama hamasa ya kuwachangia kiuchumi.- Picha zote ni kwa hisani ya http://bukobawadau.blogspot.com
Aidha ;-

Katika kusistiza kauli yake kwa vitendo juu wa walemavu katika mkoa wa Kagera kujitegemea na kujishughulisha pia  kufanya kazi mbalimbali za kujipatia kipato na kuacha kuombaomba mitaani Mkuu wa Mkoa wa Kagera ametembelea kikundi cha Walemavu (BUDAP) Nyamkazi katika mji wa Bukoba ili kujionea jinsi kikundi hicho kinavyojishughulisha.
Kikundi cha BUDAP ni kikundi cha walemavu ambao wanaendesha shughuli zao za kutengeneza bidhaa mbalimbali za mikono na kujipatia kipato kwa kuuza bidhaa hizo hasa kwa wageni mbalimbali wanaofika hapa mkoani katika sekta ya utalii. Bidhaa hizo ni ngoma za asili, vidani mbalimbali pamoja na bidhaa nyinginezo mbalimbali za mikono.
Baada ya Mhe. Massawe kufika katika kituo hicho na kujionea jinsi kikundi hicho kinavyojishughulisha na kazi za mikono amehaidi kuwatafutia mtaalam wa kutengeneza andiko la mradi ili afike katika kituo hicho na kuwatengenezea andiko ambalo atalitumia kuwatafutia wafadhili ili waweze kupata mikopo kupitia andiko hilo.
Pia amewasistiza walemavu hao kubuni miradi zaidi itakayowavutia wafadhili katika kuwasaidia. Vile vile Mhe. Massawe amewahaidi kuwa ataongea na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba ili naye awatembelee na kuona shughuli zao na jinsi ya kuwakwamua katika kupata mtaji wa kujishulisha zaidi.
Changamoto kubwa walionayo walemavu hao ni wenzao kuwakimbia na kutopenda kujishughulisha na kuishia mijini na kuendelea kuombaomba ambapo wanasema kuwa walianza kikundi na watu 20 lakini mpaka sasa wamebakia wanawake wawili na wanaume watano tu.
Mkuu wa Mkoa wa Mkoa wa Kagera alitoa kauli ya walemavua kuacha kuwa wategezi wa kuombaomba barabarani na mijini na kutafuta miradi ya kujishulisha ili wajipatie kipato cha kujiinua wao wenyewe na familia zao waka, kauli hiyo aliitoa wiki jana Alhamisi tarehe 22/11/2012 wakati akikabidhi msaada wa baiskeli mbili kwa walemavu.
Na;         Sylvester Raphael
Afisa Habari Mkoa
KAGERA @2012
 
Mapema mwezi huu wa Novemba, ngarakwetublogspot ilitembelea Muleba na kuzungumza na baadhi ya walemavu ambao,tunaamini katika msaada huo unaotolewa watahusishwa.
Mlemavu Bw Kainula ambaye ni fundi wa Kushona Viatu Mjini Muleba

Bw Twaib Abdallah Rwabasora ambaye ni fundi wa kushona Viatu,kutengeneza Simu na radio katika Kijiji cha Kasharara Muleba
  

No comments:

Post a Comment