Haya ndio yaliyojili wakati Mbunge wa Biharamulo Magharibi
Dk.Anthony G.Mbassa akichangi Hotuba ya maliasili na utalii wiki iliyopita
·
Migogoro
ya mipaka ya vijiji na maeneo ya hifadhi au maeneo tengefu.
Katika suala hili ameanza kwa kukataa
hoja ya kamati ya bunge ya maliasili na utalii ambayo imesema kuwa yawezekana
migogoro hiyo inasababishwa na wananchi kutojua maipaka ya maeneo yao na pia
badhi ya wanasiasa kutumia nafasi hiyo kukuza migogoro. Ametofautiana na hoja
hiyo kwa misingi mipaka hiyo lazima wakaazi waitambue tangu mapema, leo hii
wananchi wa kata ya kaniha, kijiji cha kaniha na mpago wameishi pale kwa zaidi
ya miaka ya 70. Mpaka wamezaliwa pale watu maarufu kama vile professa
Kulikoyera Kahigi Kanalwanda mbunge wa Bukombe, amekulia hapo mpaka ameenda
masomoni na sasa taifa linaona mchango wake bado utasema wananchi hawa
wananishi kwenye maeneo ya hifadhi? Serikali imesajili vijiji na kaniha
imesajiliwa kwa namba KGR/KIJ/694 na
mpago imesajiliwa kwa namba KGR/KIJ/695. Kama serikali ipo makini ilifanyaje
usajili wa vijiji hivi ili hali vipo kwenye eneo la hifadhi? Au kuna serikali
mbili moja inashughulikia hifadhi na moja inashughulikia usajili wa vijiji
kiasi kwamba zile document serikali moja haikujua serikali nyingine imesajili
nini? Mbaya zaidi serikali ya mkoa
imepiga marufuku wananchi kulima na wameharibiwa mazao yao, ng’ombe wao
wameibiwa na kutaifishwa na hawa wanasomesha watoto, wanategemea mazo kujikimu
ki-uchumi sasa kwa mtindo huu wataishije? Serikali imetangaza kuwa idadi ya watu
ni milioni 44.5 na kila wakifanya upimaji wa viwanja wanafanya mijini ongezeko
la watu hawa vijijini haliangaliwi je wao vijijini watajitanua kwa kuelekea
wapi? Wafugaji wafugie wapi? Nikamwambia waziri wakati anahitimisha aje na jibu
kwa wananchi hawa ambao wameambiwa wasilime na wanaishi ndani ya hifadhi.
Dk. Mbasa akaongeza kuwa kuna s/m Mpago
ambayo watoto mwaka huu wanahitimu darasa la saba. Na shule hiyo imesajiliwa na
serikali je serikali kujenga shule pale ndani haikujua kuwa lile ni eneo la
hifadhi? Kama ilijenga eneo la hifadhi serikali ilitegemea nini? Watoto wa
binadamu wakasome au swala na pundamilia ndio wakasome hapo ndani ya hayo
madarasa? Akamwambia waziri kuwa anahitaji i kupata jibu ni lini wizara ya
maliasili na utalii watakaa na wizara ya ardhi nyumba na makazi kuja kutatua
mgogoro huu walioutengeneza wao.
·
Suala
la pili aliongelea kuhusu hotuba ya waziri wa maliasili na utalii kuwa
zitafanyika doria 100000 (laki moja) katika maeneo ya hifadhi na mapori ya
akiba.
Katika kuchangia hili alisema hakika hizi
si doria za kuchunga au kuhifadhi wanyama wetu, bali ni doria kwa ajili ya
kufukuza ng’ombe walioko jirani na mipaka ya vijiji na kuwaingiza hifadhini na
hatimaya ekuwatoza pesa wananchi pasipo sababu yoyote. Akamwambia waziri
akumbuke alivyofanya ziara jimboni kwake(Biharamulo), taarifa aliyompa wakiwa ofisini
kwa DC(Mkuu wa wilaya) na mambo waliyomwambia akiwa kwenye mkutano wa hadhara
katika kijiji cha Ruziba, wananchi walieleza kinagaubaga kuhusu matatizo yanayo
wasibu na mipaka yao na game reserves. Wanavyonyanyaswa na askari wa
wanyamapori, wakikamatwa japo kwa kusingiziwa wanavyopigwa, akaomba serikali
itoe kauli kwa nini hawa wanafanya kazi kinyume na sheria, utaratibu na kanuni
za kazi zao? Wao wanapaswa kulinda wanyamapori na mipaka yao na si kazi ya
kuchunga mifugo ya watu ndani ya hifadhi au kukamata ng’ombe kana kwamba wao ni
waajiliwa wa wizara mifugo na uvuvi.
·
Kuhusu
suala la fidia kwa wale wanaoharibiwa mashamba yao na wanyama au kuuawa na
wanyama wakali.
Hapa Mh. Mbunge alihoji wizara
kutotoa nyaraka kuhusu fidia wanayopawsa kulipwa waale ambao wameharibiwa
mashamba yao au kuuawa na wanyama hawa. Mambo haya hayapo wazi, lakini mtu
akimdhuru ngedere inakuwa hoja wakati nyani akimdhuru binadamu linakuwa jambo
la kawaida. Hivyo akaomba wizara husika kutoa nyaraka hizo ikiwezekana na
wabunge wapewe ilikutetea wananchi wao.
OPERESHENI YA WAFUGAJI HARAMU KAGERA.
“Mnamo mwezi novemba 2012 mkoa wa Kagera uliendesha operation
ya kuondoa Wafugaji haramu ndani ya hifadhi ya hifadhi ya Burigi
a) Je, ni wagugaji haramu wangapi walibainika
katika operarion hiyo?
b) Je, serikali imewapa fidia gani wale
walioharibiwa mashamba yao na mifugo hususan kata ya Lusahunga na Kaniha?”
WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII
Mheshimiwa spika,
Kabla ya kujibu swali la MHESHIMIWA DKT ANTONY GERVASE
MBASSA(MB) BIHARAMULO MAGJHARIBI naomba kutoa maelezo yafuatayo:
Ni kweli Wizara yangu mwezi Novemba, 2012 ilifanya doria
maalumu kwa kushirikiana na Kamati ya Ulinzi na usalama ya mkoa wa Kagera
(Jeshi la polisi,magerza, uhamiaji, TAKUKURU na JWTZ) ili kuwaondoa wafugaji
haramu ndani ya mkoa wa Kagera hususan Wilaya ya Biharamulo, Muleba, karagwe na
Ngara. Operation hii ilipewa jina la OMAKA- Okoa Mazingira Kagera. Umuhimu wa
operarion hii ulitokana na ukweli kwamba, kulikuwepo na uingizaji wa mifugo (hasa
ng’ombe), upasuaji mbao, uchomaji wa mkaa,shughuli za kilimo na uchimbaji wa
madini isivyo halali ndani ya Hifadhi ya Misitu ya Mapori ya Akiba ya
wanyamapori.
Mheshimiwa spika,
Baada ya maelezo hayo sasa naomba kujibu swali la MHESHIMIWA
DKT ANTONY GERVASE MBASSA(MB) BIHARAMULO MAGHARIBI lenye sehemu (a) na(b) kama
ifuatavyo;
a) Katika Operesheni hiyo, wafugaji wane
walikamatwa ndani ya Mapori ya Akiba ya Burigi, Biharamulo na Kimisi wakiwa na
jumla ya ng’ombe 466.
b) Kwa mujibu wa Sheria ya Kuhifadhi
Wanyamapori na 5 ya mwaka 2009 na kanuni ya Kifuta jasho na kifuta machozi ya
mwaka 2011, Serikali haitoi kifuta jasho kwa wafugaji haramu na wavamizi
wanaolima ndani ya maeneo ya hifadhi.
“HAYO NDIO MAJIBU YA WIZARA KULINGANA NA SWALI UNAVYOLIONA
HAPO JUU. FIKIRIA MAZINGIRA KAMA HAYO NA BAHATI NZURI ULIFIKA KWENYE MAENEO
HUSIKA NA UKAONA HALI HALISI YA MAZAO YALIVYO HARIBIWA, NYUMBA ZILIVYOCHOMWA
MOTO.”…. Dk Mbassa
Pamoja na majibu ya swali, Dk Mbassa alianza kuumuliza N/W
kama majibu huwa wanayasoma kabla ya kwenda kuyasoma bungeni!
Alimuuliza N/W “kweli operesheni amabayo imegarimu kiasi cha
zaidi ya 400 milioni Tshs halafu unakamata waafugaji 4, je zoezi hilo
lilizingatia thamani ya pesa na tija iliyopatikana katika zoezi hilo?”
Mwisho akauliza wizara inatoa kauli gani kwa waliokamatiwa
mifugo kwa maana ya kuifukuzia ndani ya hifadhi ili wawatoze pesa wananchi! Swali
ambalo halikuwa na Jibu.
Hata hivyo,Mbunge huyo, ameahidi hivi karibuni akimaliza
Vikao vya Bunge kufika jimboni kuzungumza na wananchi kuwapelekea majibu aliyopewa.
Kila la
kheri Dk.Anthony Gervase Mbassa MB Biharamulo Magharibi. Nasi tunakutakia
Mafanikio katika uwakilishi wa wananchi.
No comments:
Post a Comment