August 6, 2013

Wahamiaji haramu watishia maisha ya wananchi MulebaNa Shaaban Ndyamukama Agost 06,20013

MULEBA:WANANCHI wa kata za Rutoro na Ngenge katika wilaya ya Muleba Mkoani Kagera maisha yao yako hatarini baada ya kuvamiwa na wahamiaji haramu na wenye mifugo kisha kulishiwa mashamba yao 

Mbunge wa jimbo la MULEBA Kaskazini Charles Mwijage ameliambia gazeti hili jana kuwa wahamiaji hao waliingia katika kata hizo tangu Rais Kikwete atoe agizo la wahamiaji haramu kuondoka nchini  ndani ya siku 14 kabla ya kuanza msako dhidi yao

Mwijage amesema kuwa mifugo iliyoshambulia mashamba ya wananchi wa kata hizo ni takribani 300  na walitokea eneo la pori la burigi kilomita 45 kutoka karika kata hizo

Alisema kuwa wananchi kwa sasa watakumbwa na janga la njaa kwani mazao waliyokuwa wakitegemea katika yameliwa na mifugo hiyo na wengine wanadhaniwa kuwa majangiri wanaoingia katika hifadhi na kupora maliasili za Taifa

“Ifanye nguvu za ziada katika kuwaondoa wahamiaji haramu kwani wana mtandao mkubwa na wanaendelea kuwa na dharau hata kwa  na vyombo vyake vya dola”
Amesema pia wahamiaji hao wanatishia maisha wanaowanyoshea vidole na kuwakemea kupitia mikutano ya wananchi hivyo ni jukumu la serikali kuhakikisha watu wa namna hiyo wanatiwa kwenye mkondo wa sheria

Kwa mujibu wa Mbunge huyo ni kwamba amemtaarifu waziri mkuu na wizara ya mambo ya ndani kuhaikisha wanaimarisha usalama wa raia na mali zao pasipo kutafuta maneno kupitia majukwaani

Hivi karibuni Rais Kikwete akiwa ziarani mkoani Kagera alitoa siku 14 kwa wanaomiliki silaha kinyume cha sheria kujisalimisha na silaha zao ama kuondoka nchini hasa katika mikoa ya Kagera na Kigoma

Inakadiliwa mkoani Kagera  unao wahamiaji haramu zaidi ya 35 000 na wamekuwa wakishirikiana na watanzania wasio waaminifu kimaadili na kuteka magari kisha kupora mali za abiria pamoja na  wenye mifugo kuharibu mashamba ya wakulima. MWISHO

No comments:

Post a Comment