August 6, 2013

HALMASHAURI YA WILAYA YA MULEBA YATOA VYOMBO VYA USAFIRI KWA WATUMISHI WA VIJIJI NA KATA

Baadhi ya maafisa watendaji wilayani Muleba wakizijaribu pikipiki walizogawiwa

Baiskeli kwajili ya wahudumu wa afya Vijijini

Mwenye tai nyekundu ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Muleba Bw.George Katomelo

                                Mwenyekiti wa halmashauri Bw.George katomelo akikabidhi Pikipiki

M/Kiti wa halmashauri akizungumza na Vyombo vya habari baada ya mgao huo

Diwani wa kata ya Muleba Mjini Bw. Hassani Millanga

Wahudumu wa afya vijijini wakipokea Baiskeli za Kazi
 
Maafisa watendaji wa kata wakiwa tayari kuondoka na Pikipiki zao

Kushoto ni Afisa habari wa Halmshauri ya Muleba

madiwani wa H/W Muleba katika moja ya Vikao vya Baraza lao

Mwenye shati jeupe ni Charles Mwijage Mb. wa Muleba kaskazini akiwa katika kikao cha Baraza

Majengo ya Ofisi za halmashauri ya Muleba yakikarabatiwa

Wakuu wa Idara ya H/W Muleba wakisoma makablasha ya Kikao


Watumishi wa kata na vijiji wapatiwa vyombo vya usafiri Muleba
Na Shaaban Ndyamukama Agost 05,2013

MULEBA: HALMASHAURI ya Wilaya ya Muleba mkoani Kagera  imewapatia vyombo vya usafiri watumishi wake  ngazi ya kata na vijiji  ili waweze kutekeleza majukumu na malengo ya halmashauri hiyo  kuleta maendeleo ya wananchi kwa haraka.

Mkurugenzi wa Halmashauri wa wilaya hiyo Oliva Vavunge amesema  hayo Agosti 01,kuwa watendaji wa kata 18 wamepatiwa pikipiki zenye thamani ya Tsh. 39 mil na wahudumu wa Afya vijijini 45 wamepatiwa Baiskeli  zilizogharimu Tsh.8.1 mil

Vavunge amesema  kuwa fedha zilizotumika kununua vyombo hivyo vya usafiri ni kutoka katika mapato ya ndani ya halmashauri hiyo na watumishi  hao wamekopeshwa na watakuwa wakikatwa fedha kutoka katika mishahara yao ili kwa awamu nyingine watendaji wa kata 13 waweze kukopeshwa

Aidha amesema halmashauri kupitia idara ya kilimo imenunua trekta kwa kiasi Tsh.milioni 42 ambapo kwa atakayelihitaji kulitumia kwa kilimo na atalikodi kwa ekari moja Tsh.60,000/=.

Naye Afisa mtendaji wa kata ya Biirabo Boaz Musasa ameshukuru kwa niaba ya wenzake kupatiwa pikipiki na kwamba katika kata yake amehudumia vijiji vyenye maeneo mapana yaliyo na mabonde na milima.

Akikabidhi  vyombo hivyo Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Muleba Bw George katomelo amewahimiza kuhakikisha watumishi hao wanavitumia kwa malengo yaliyokusudiwa licha ya kuwa mali yao baada ya makato katika mishahara yao.             MWISHO

No comments:

Post a Comment