November 4, 2013

Makaburi 40 yafukuliwa ili kupisha ujenzi wa kizuizi cha mpaka wa Tanzania na Burundi


Hivi ndivyo mambo yalivyokuwa,wananchi wakishiriki kufukua makaburi ya ndugu zao kupisha ujenzi huo.


Picha:- kwa hisani ya Dotto Jasson Bahemu na Simon Dionizy

Kijana ambaye jina lake halikufahamika mara moja akifukua kaburi


wananchi wakitoa mabaki ya mwili wa marehemu katika kaburi kwenda kuyazika upya

wananchi wakishuhudia zoezi la kuhamisha miili ya marehemuZoezi la kuhamisha makaburi 40 kutoka katika eneo la ujenzi wa kizuizi cha mpaka wa Tanzania na Burundi eneo la Nzaza kata ya Kabanga wilayani Ngara Mkoani Kagera limefanyika November 04,2013. 

Katika zoezi hilo mabaki ya milii ya marehemu imefukuliwa na kuzikwa upya
Diwani wa kata ya Kabanga Bw Said Soud amesema kuwa zoezi hilo limefanyika kwa amani

Bw Soud amesema kuwa wanafamilia wa Marehemu hao wameonyesha ushirikiano wa kutosha, licha ya  kuwepo changamoto za matumizi ya vifaa duni  vya kufukua makabuli na kubeba mabaki ya miili ya marehemu

www.ngarakwetu.blogspot.com imezungumza na baadhi ya wakazi wa eneo hilo ambapo wengi wamesema serikali imefanya jambo la maana kuwapatia fidia ya fedha za kuhamisha makaburi hayo na kuzikwa upya kwa ndugu zao

No comments:

Post a Comment