November 17, 2013

Wahitimu wa elimu waaswa kulinda maadili


Mkuu wa wilaya ya Biharamulo Bw. Richard Mbeho


Wahitimu

Mkuu wa wilaya akiwa na Mkuu wa Seminari ndogo ya Katoke
                                                                 
Wanafunzi wa katoke seminari


Mapadre, katika Misa takatifu kama sehemu ya mahafali
  
Na Shaaban Ndyamukama November 17, 2013
BIHARAMULO: Wahitimu wa ngazi mbalimbali za elimuwametakiwa kutumia maadili waliyopata katika shule zao kulinda Amani na kuleta maendeleo kwa kutumia  taaluma zao ikiwa ni pamoja na kujiendeleza kuongeza ujuzi na maarifa.
Mkuu wa wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera Bw Richard Mbeho ametoa wito huo Nov 16 katika mahafali ya 40 ya wahitimu wa kidato cha nne katika shule ya seminari ya katoke  inayomilikiwa na jimbo katoliki la Rulenge  mkoani Kagera.  
Bw Mbeho amesema kuwa pamoja na kutumia taaluma mbalimbali hawana budi kuwa makini na utandawazi kwenye  mazingira yao kwani unaweza kuchangia kujiingiza katika vitendo viovu na kuhatarisha usalama wa maisha yao.
“Jiepushe na rushwa kwa kutaka mali,  madaraka,ngono na hatimaye kujiingiza kwenye vitendo vinavyoweza kuhatarisha usalamana Amani kupitia njia za utandawazi”.Alisema Mbeho
Amewahimiza na wahitimu kujiendeleza kitaaluma na  wazazi kuendelea kutoa malezi kwa watoto wao  ili waendelee kutegemewa na taifa kwa kutoa huduma mbalimbali ndani ya jamii zao.
Awali katika ibada ya misa kwa wahitimu hao mkuu wa shule ya seminari ya katoke padre Frolian Tuombe amesema shule hiyo inatoa masomo yote yakiwemo ya  ya kiroho kwa kulinda maadili i kwa nadharia na vitendo
Padri Tuombe amewataka wahitimu kufanya kazi kwa uadilifu kwa mujibu wa Imani yao kwa kuzingatia utii wa sheria kanuni za utumishi na kuwajibika bila kwa kulinda haki pasipo kuwa na uonevu wala ubaguzi wa aina yoyote
Katika mahafali hayo zaidi ya Tsh mil 2.59/- zimechangwa na wazazi wa wanafunzi waliohitimu kidatocha nne  mwaka huu katika shule hiyo ambapo fedha taslimu ni Tsh 775,200 ili  kupunguza changamoto mbalimbali zinazoikabili jumuia ya shule.

No comments:

Post a Comment