November 5, 2013

KAULI ZA WIZARA YA ELIMU ZINAWACHANGANYA WANAOFANYA MTIHANI

Mjumbe wa kamati tendaji ya Chama Cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA wilayani Ngara Bw. John Simon  Malanilo



Mjumbe wa kamati tendaji ya chama cha na maendeleo CHADEMA wilayani Ngara Bw Bw. John Simon  Malanilo amesema kitendo cha serikali kujichanganya kuhusu mpangilio wa madaraja kinaweza kuwachanganya watahiniwa wa kidato cha nne ambao kwa sasa wanafanya mitihani yao ya kuhitimu elimu ya sekondari nchini

Bw Malanilo ametoa kauli hiyo alipozungumza na Radio Kwizera  ya mjini Ngara kuhusu kauli za maafisa wa juu wa wizara ya elimu nchini ambapo hivi karibuni Katibu mkuu wa wizara hiyo Prof  Sifuni Mchome alitangaza kuwepo kwa daraja hadi la tano huku Naibu Waziri Philip Mulugo akisema leo kuwa hakuna daraja la 5 badala yake litakuwepo daraja la sifuri kama kawaida

Amesema kukinzana kwa viongozi hao kunaonesha kutokuwa na mipango mizuri katika kuchochea maendeleo ya elimu nchini na kwamba kinachoshusha ubora wa elimu nchini ni mipango isiyo madhubuti katika wizara ya elimu

Aidha Bw Malanilo amesema malumbano ya mpangilio wa madaraja kwa sasa hayana tija ambapo ameishauri serikali kuwekeza katika kuwalipa walimu vizuri na kwa wakati, kuajiri walimu wa kutosha, kuboresha vifaa vya kufundishia na kujifunzia na kuboresha makazi ya walimu

1 comment:

  1. Asante kwa ufafanuzi.Napenda kufahamu,huyu John Simon Malanilo ni ndugu yake na Peter Bujari?Na,je kwa jina jingine na yeye anaitwa John Bujari?Nitafurahi kama ndugu yangu mwandishi Juvenali nitapata majibu haya.Maana huyu jamaa kama vile namfahamu alikuwa Mwalimu wangu.Ni mtu makini sana japo nilikuwa bado mdogo,ila alikuwa na haiba ya uongozi na kufahamu mambo.NWAKILISHA

    ReplyDelete