January 27, 2014

CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)Kimesema kuwa serikali haina budi kuwa wajibisha kwakuwafikisha mahakamani maramoja baadhi ya maafisa wake wanaotuhumiwa kwa ufisadi Wito huo wa CHADEMA umetolewa na viongozi mbali mbali wa ChDEMA katika mikutano ya hadhara iliyofanyika katika wilaya za mkoa wa kagera ikiwa ni mwendelezo wa operesheni maalumu ya MOVEMENT FOR CHANGE M4C PAMOJA DAIMA,huku kikiwahimiza wananchi kuwaibua na kuwaweka hadharani baadhi ya maafisa wanaotumia ofisi zao kwa masilahi binafsi Mmoja wa viongozi wa CHADEMA walioibua hoja hiyo ni pamoja na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Mbunge wa Jimbo la Ubungo Bw.John John Mnyika ambaye alisema kuwa anashangazwa kuwaona baadhi ya mafisadi wakiendelea kula maisha mitaani badala ya serikali kuwafungulia mashitaka Mbunge huyo na waziri kivuli wa nishati na madini ameyataja baadhi ya makampuni hewa ambayo yametumiwa na maafisa wa serikali kujinufaisha kwakutumia mikataba mibovu kuwa ni pamoja Richmond, IPTL,Net Group,Dowans,Songas,Symbion nakadhalika Alisema serikali inapaswa kuwachukulia hatua kali mafisadi hao kwa madai kuwa wamesababisha ugumu wa maisha kwa wananchi,kwakuwa kutokana na ubadhirifu wao gharama za maisha zinazidi kuwa kubwa huku Taifa likikosa kodi kutoka katika makampuni ya wageni walioingia mikataba mibovu Mnyika alisema licha ya kwamba mafisadi hao walitajwa katika kashfa hiyo ya ufisadi, lakini hawajachukuliwa hatua yeyote “Serikali kama ingekuwa sikivu kwa wananchi wake,ilitakiwa kuwachukulia hatua kwa kuwafikisha mahakamani mafisadi kwakuwa ndio wanapelekea watanzaniakuishi katika maisha magumu.Kama kuna Nchi ambayo imejaliwa rasilimali nyingi ni Tanzania ila haziwanufaishi watanzania,” alisema Mnyika. Myika pia alizungumzia suala la Umeme kwakusema kuwa gharama za nishati hiyo zimeongezeka sana kutokana na mikataba mibovu Katika mikutano ya Ngara,Bukoba Mjini,Biharamulo,na Geita Mwenyekiti Mwenyekiti taifa wa CHADEMA Mh. Freeman Mbowe ambaye ni Mbunge wa jimbo la HAI Chama chke hakiko tayari kuivumilia serikali ikiendelea kuwaacha viongozi hao pasipo kuwachukulia hatua na kwamba kitaendelea kuishitaki kwa wananchi Geita wa Mpokea MBOWE kwa Mabango ya ZITTO,wampa uwaziri mkuu huku SLAA akitajwa kuwa Rais Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA taifa Mh. Freeman Mbowe amepokelewa kwa shangwe mjini Geita,huku wananchi wakimtaja kuwa ni waziri Mkuu Hayo yamejiri katika mkutano wake aliofanya mjini Geita akitokea mkoani kagera alikohutubia mikutano ya hadhara katika wilaya za Ngara,Biharamulo,Kagera,Bukoba mijini na Vijijini,Muleba na kwingineko Licha ya shamra shamra za kumpokea mwenyekiti huyo pia walibeba mabango yaliyosomeka”Katiba Mpya ni lazima,CHADEMA kwanza Zitto baadaye” Katika hatua nyingine,wananchi hao walionesha hamu ya kumuona katibu mkuu wa chama hicho Dk.Wilbroad Slaa walipopaza sauti zao wakisema,tunamtaka rais Dk. Slaa

No comments:

Post a Comment