July 16, 2016

MIUNDOMBINU DUNI YA MAJI NA UONDOAJI TAKA NI CHANZO CHANZO CHA KIPINDUPINDU


Mtaalam wa miradi wa UNESCO anayeshughulikia masuala ya maji na makazi  kutoka Paris –Ufaransa Dkt.Alexandros Makarigakis akifungua Mkutano
DAR ES SALAAM
Wizara ya maji na Umwagiliaji imetaja tatizo la  miundombinu bora ya maji na Mifumo ya uondoshaji wa taka katika maeneo mbali mbali kuwa chanzo cha Magonjwa ya mlipuko hasa Kipindupindu ambacho ni changamoto kwa maendeleo ya Taifa

Mkurugenzi wa rasilimali maji katika wizara hiyo Dkt. George Lugomela amesema hayo wakati akitoa taarifa katika Mkutano ulioandaliwa na shirika la maendeleo ya Elimu,Sayansi na Utamaduni UNESCO uliofanyika katika Hoteli ya Protea Jijini Dar Es Salaam

Dkt.Lugomela amesema mkoa wa Dar Es Salaam pekee una  asilimia 10 ya Mfumo wa maji safi na uondoaji wa taka katika mitaa  hali inayokwamisha mapambano dhidi ya ugonjwa wa Kipindupindu

Kwa Upande wake Mtaalam wa miradi wa UNESCO anayeshughulikia masuala ya maji na makazi  kutoka Paris –Ufaransa Bw.Alexandros Makarigakis amesema Shirika hilo limedhamilia kukomesha vifo vitokanavyo na Kipindupindu  kwasababuza  ukosefu wa maji safi na salama ya kunywa, Miundombinu mibovu ya Maji mifumo yake.
Washiriki wakiendelea na Mkutano



www.ngarakwetu.blogspot.com

No comments:

Post a Comment