July 11, 2016

Rais Jacob Zuma ziarani Ufaransa

François Hollande, Rais wa Ufaransa, na Jacob Zuma, mwenzake wa Afrika Kusini, picha iliyopigwa mwaka 2013.
SOURCE:http://sw.rfi.fr/
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma anaanza, Jumatatu hii, Julai 11, ziara ya kikazi nchini Ufaransa. Rais Zuma atakutana na Rais wa Ufaransa François Hollande Jumatatu hii jioni.
Siku ya Jumanne, viongozi hawa wawili watatembelea katika eneo la Somme kuhudhuria sherehe za miaka mia moja ya vita vya Delville Wood, ambapo zaidi ya askari 3,000 wa Afrika Kusini walikabiliana na askari wa Ujerumani katika Vita Kuu vya Dunia. Kisha viongozi hawa watajadili suala la ushirikiano wa kiuchumi. Ufaransa na Afrika Kusini wanashirikiana kibiashara kwa kiasi kikubwa licha ya mahusiano mara nyingine kudorora.
Afrika Kusini na Ufaransa wana uhusiano mkubwa. Kwa miaka mingi, Paris inaisadia Afrika Kusini, pamoja na soko lenye uwezo mkubwa na kufika hadi kusini mwa Sahara. Lakini upande wa Pretoria, wanapuuzia. ANC, chama tawala tangu mwisho wa ubaguzi wa rangi, kinaendelea na mtazamo kujihami dhidi ya nchi za Magharibi, hasa Ufaransa kinaituhumu kuingilia masuala ya ndani ya nchi za Afrika, kutokana na ushawishi wake nchini Cote d'Ivoire, Madagascar na kuingilia kijeshi nchini Mali.
Hali hii liojitokeza hasa katika uchaguzi wa rais wa Tume ya Umoja wa Afrika. "Ilikuwa inayoonekana katika uchaguzi wa Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika, miaka 4 iliyopita. Afrika Kusini, katika kampeni yake ya kuunga mkono mgombea wake, ilimshtumu mshindani wake, Jean Ping, raia wa Gabon, kuwa kibaraka wa Ufaransa. Ikiongeza kuwa Ufaransa iliingilia masuala ya ndani nchini Cote d'Ivoire na Mali. Kulikua kila mara na uhusiano mgumu, "anasema Peter Fabricius, mshauri katika Taasisi ya Mafunzo ya Usalama. Kwa mujibu wa Fabricius, Afrika Kusini inaelewa. Afrika Kusini inatambua kwamba Ufaransa inaweza kuwa mshirika muhimu barani Afrika, ikiwa ni pamoja na mshirika wa kiuchumi, ambaye inatakiwa kutopuuziwa.
Matarajio ya uwekezaji wa raia wa Ufaransa
Afrika Kusini inahitaji uwekezaji. Ukuaji unatarajiwa kufikia 0.6 % mwaka huu na mashirika kadhaa binafsi yatishia kupunguza ushirika wao katika kiwangu cha juu. Wanauchumi wanakubaliana na hilo, kwa nchi ina mengi ya kutoa maendeleo katika sekta ya benki, mawasiliano, usafiri, malighafi. Lakini nchi hiyo inahitaji zaidi hisa, anasema Ian Cruickshanks, katika matarajio ya kuondoka kwa Uingereza katika Umoja wa Ulaya.
www.ngarakwetu.blogspot.com

No comments:

Post a Comment