June 25, 2017

UZINDUZI WA DAYOSISI BIHARAMULO,ASKOFU WA KWANZA VITHALIS YUSUPH SUNZU




Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikan Tanzania Dk.Jacob Chimeledya ametaka serikali kufanya marekebisho  baadhi ya sheria ambazo zimekuwa kandamizi kwa jamii pamoja na kuiangazia upya  mikataba yote inayohusu rasimimali za umma yakiwemo madini ili ziwe na manufaa kwa wananchi.

Askofu Chimeledya ametoa kauli hiyo  kwenye ibada ya kuzindua dayosisi Mpya ya Biharamulo na kuwekwa Wakfu kwa Askofu wa kwanza wa Dayosisi hiyo Askofu Vithalis Yusuph.

Bila kutaja sheria husika ,Alisema baadhi ya sheria zikiwemo sheria paamoja na mikataba iliyoingiwa na serikali inaumiza wananchi na hivyo ifaa ifanyiwe marekebisho ili rasilimali hizo ziwanufaishe wananchi.

Alisema Tanzania bado ina mikataba mibovu hasa katika sekta ya madini kwani rasilimali hizo haziwanufaishi wananchi kama zilivyotolewa na mwenyezi Mungu kwa ajili wanadamu.

Alishauri serikali kuwa, kama kuna mikataba iliyoingiwa ni mibovu heri ikafanyiwa marebisho kuliko kuendelea kupoteza rasilimali nyingi za watanzania kwa manufaa ya watu wachache.

Aidha kusuhu sheia za mwanamke Askofu huyo alisema katika sheria nyingine mbovu ni sheria ya motto hasa wa kike ambapo baadi yake zimekuwa kandamizi kwa motto wa kike kwani zimekuwa hazimlindi mtoto wa kike katika mazingira ya leo na hivyo kuwa kandamizi kwake.

“Tunaomba sheria zirekebishwe zikiwemo za kulinda haki za mtoto wa kike katika mazingira ya leo.Tunaona baadhi ya sheria haziendani kabisa na utu wa kibinadamu na zimekandamizi kwa mtoto hasa wa kike”alisema Askofu.

Hata hivyo,alisema kanisa linaunga mkono juhudi za serikali inayoongozwa na Rais John Pombe Magufu katika kupigania rasilimali za nchi yakiwemo madini,na kuongeza kuwa kanisa litaendelea kumuombea.

“Tunatambua kazi nzuri zinazofanywa na rais Wetu Magufuli za kupigania rasimali za nchi,lakini cha msingi tunaomba kasoro zilizopo kwenye mikataba ya madini na sheria zingine mbovu zifanyiwe marekebisho…zipo kanuni nyingi ambazo zimetumifika hapa tulip oleo”alisema Askofu.

Aidha,Askofu wa Dayosisi ya Biharamulo katika Hotuba yake mara baada ya kusimikwa kuwa Askofu wa Dayosisi hiyo ya 28,alisema Watanzania walio wengi wanaishi katika mazingira magumu na ili kuondokana na hali hiyo Viongozi wa dini na serikali wana wajibu wa  kuwahudumia wananchi kwa ushirikiano.

Katika kuonyesha kukerwa na tabia za utumikishwaji wa watoto,Askofu Yusuph alisema, kanisa la Angilikani Dayosisi ya Biharamulo halitakubali kuona motto anatumikishwa katika ajira hatarini za migodini,kwenye migahawa na kuchunga mifugo.

Akizungumzia changamoto za wananchi wa Biharamulo mbele ya Mgeni Rasim Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga,alisema wakazi wa wilaya hiyo wanakabiliwa na tatizo la upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama.

Alisema kutokana na hali hiyo baadhi yao wamekuwa wakishinda usiku wamanane wakitafuta huduma ya maji sehemu mbalimbali na hata maji wanayotumia hayako salama kwa ajili ya Afya zao.

Aliongeza kuwa kanisa litashirikiana na serikali kuhakikisha huduma ya maji safi na salama kutoka Ziwa Victoria inapatikana kwani kanisa hilo linatambua juhudi za serikali za kuwaletea wananchi maendeleo.

Kwa upande wake Mgeni Rasmi Ezekiel Kyunga ambaye pia ni Mkuu wa mkoa wa Geita aliyemwakilisha Rais wa John Pombe Magufuli katika Hafla hiyo alisema,serikali itahakikisha inashughulikia kero za wananchi na kuwataka viongozi wa dini kutoa ushirikiano katika mkakati wa serikali ya awamu ya tano ya kuwaletea wananchi maendeleo.

Amewataka vongozi dini kuhakikisha wanatumia nafasi zao katika kueneza injili ili kuwa Taifa lenye kumpendeza Mungu na kupunguza uharifu unaojitokeza.

Kuhusu maji,alisema serikali iko tayari kushirikiana na kanisa hilo kuhakikisha wananchi wa Biharamulo wanapa huduma ya maji safi na salama,na kudai kuwa anatambua juhudi za kanisa hilo kutumia rasilimali fedha kuwahudumia wananchi ikiwemo elimu,Afya na Maji.

Shughuli za kusimikwa kwa Askofu huyo zilifanyikwa kwa kuzingatia miongozo ya kanisa hilo ikiwemo kula kusoma hati mbalimbali za viapo ili kulitumikia kanisa hilo.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa dini kutoka dayosisi za Tanzania viongozi wa serikali wakiwemo wakuu wa wilaya pamoja waumini wa dayosisi za Biharamulo na Kagera.
Mwisho


www.ngarakwetu.blogspot.com

No comments:

Post a Comment