August 21, 2012

WANAUME WENGI NGARA WANA WANAWAKE ZAIDI YA MMOJAUtafiti wa shirika lisilokuwa la kiserikali  linalojihusha na utoaji wa elimu  kwa  familia, Global  Family  Enlightment  Organization  umebaini kuwa zaidi ya  asilimia  88 ya wanaume walio katika ndoa  mkoani Kagera wana wake wengine  pembeni maarufu kama nyumba  ndogo.
Mkurugenzi  wa shirika hilo  mkoani kagera  Bw  Inocent  Bideberi  amesema  kuwa  hali hiyo inarudisha  nyuma maendeleo ya familia kwani wahusika wanashindwa kuhudumia familia zao
Bw  Bideberi  amesema  utafiti umeonesha kuwa   wanaume wangi  wamekuwa na mwanamke zaidi ya mmoja.
Amesema shirika lake limeandaa  mpango wa kuanza kutoa elimu  kwa jamii   ili kufahamu madhara ya kuwa na nyumba ndogo kwa familia. 
           Source: www.radiokwizera.com

No comments:

Post a Comment