October 15, 2012

Wajasiriamali wa Ngara wakisubiri Usafiri wa Maloro kupeleka mazao wilayani Kahama mkoani Shinyanga

Ndizi kutoka Ngara, ambalo ndio zao kuu la Biashara


Halmashauri Ngara itatue migogoro ya Ardhi kwa wananchi wake
Na Shaaban Ndyamukama.Ngara
Halmashauri ya wilaya ya Ngara mkoani Kagera imeshauriwa kuondoa migogoro ya arhi kwa wananchi wake kwa kutafuta jingo na kuanzisha baraza la ardhi ili kuondoa changamoto zinazowakabili wakulima na wafugaji katika halmashauri hiyo
Mbunge wa jimbo la Ngara  Deogratias Ntukamazina alitoa ushauri huo wakati akiongea na baraza la madiwani hivi karibuni wilayani Ngarakwa kuelekeza halmashauri hiyo kutafuta mahali palipo karibu na wananchi kijiografia kujenga jengo kwa ajili ya kuanzisha baraza la ardhi litakalosaidia wananchi kupunguza kero za mashamba
Bw Ntukamazina alisema kuwa   wananchi wanayo migogoro ya ardhi wilayani ngara kwa kugombania mipaka ya mashamba na kusumbuka kutafuta suluhu kwa kulazimika kwenda wilayani chato na hutumia gharama kubwa kupata haki zao
Alisema kuwa kama jengo litatolewa na halmashauri wizara ya ardhi na maendeleo ya makazi itatuma wataalamu wa kulikagua na kutoa ushauri wa maboresho ili kesi mbalimbali za ardhi ziweze kusikilizwa na kutatua kero zinazowakabili wananchi.“Migogoro ya ardhi kwa wananchi wetu imekuwa ikisikilizwa na baraza la ardhi la kata lakini wajumbe wake baadhi yao wamekuwa hawana ujuzi katika sheria na kusababisha wengi kutaka rushwa na kuwakosesha haki waliozistahili kupata haki zao kihalali”.Alisema Ntukamazina
Alidai wilaya ya ngara ina ardhi yenye rutuba na wananchi wanaojishughulisha na kulimo cha ndizi hasa tarafa za kanazi na Nyamiaga huku tarafa za Rulenge na Murusagamba wakilima maharage karanga ulezi mtama na matunda mbalimbali pamoja na ufugaji wenye kulinda na kuhifadhi mazingira.Hata hivyo mbunge huyo aliwasihi wananchi kutumia vema ushauri utakaotolewa na baraza la ardhi la wilaya litakapopatikana katika kuhakikisha wanadumisha amani na mshikamano katika vijiji badala ya kusababisha vurugu kwa watakaoshindwa kupata haki zao kwa mujibu wa sheria.Ends

No comments:

Post a Comment