November 16, 2012

Huyu ndiye Mkuu wa wilaya ya Ngara

Aliyesimama na Microphone mkononi ndiye Mkuu wa wilaya ya Ngara-Costantine Kanyasu

Aliyesimama katikati mwenye mawani. Bw.Costantine Kanyasu. Mkuu wa wilaya ya Ngara-Kagera

Nafikisha pongezi za baadhi ya wananchi wa Ngara kwako Mh. Mkuu wa wilaya. kwa kipindi ambacho umeshika madaraka wilayani Ngara, wananchi wameonesha kukubali utendaji kazi wako hasa kushughulikia kero za uvamizi wa wafugaji katika maeneo ya wakulima,sanjari na Oparesheni maalumu ya kuwaondoa wafugaji haramu.

Kwa mafanikio haya. www.ngarakwetublogspot.com inakumbusha kuwepo kwa wahamiaji haramu(wahamaiaji kutoka nje ya Tanzania) hasa Nchi jirani ya Burundi ambao wanaishi katika maeneo mbali mbali ya wilaya ya Ngara.

Tunakuomba ili kuepusha madhara yatokanayo na watu hao,tafadhali elekeza nguvu katika suala hilo. Vijiji vingi vimejaa watu hao. Wapo baadhi ya viongozi wa kata,vijiji na Vitongoji wanashiriki kuwahifadhi wahamiaji. wanatumika katika shughuli zakilimo. "tukumbuke kuishi na wahamiaji kama hao ambao hawako kisheria wala taratibu ni sawa na kuishi na BOMU ambalo hujui litalipuka lini! na madhara yake yatakuwaje"

Tunaamini,Mkuu utalishughulikia hilo. Nasi tutatoa ushirikiano

No comments:

Post a Comment