November 13, 2012

WASWAHILI WALISEMA, PENYE NIA PANA NJIA.



Awilo Longomba


WASWAHILI WALISEMA, PENYE NIA PANA NJIA.

NI MSEMO WENYE KUTIA MOYO….

Naomba niutolee Mfano mzuri msemo huo kwa Mwanamuziki kutoka jamhuri ya kidemokrasia ya Congo DRC zamani ikijulikana kama ZAIRE ambaye alianza kama Mpiga Ngoma hadi katika Usupa staa…………
Wengi tumemzoea kwa jina la Awilo Longomba. Huyu ni miongoni mwa wanamuziki wanaotamba Afrika na hata nje ya bara hili. Ndoto zake katika Muziki zilianzia katika upigaji wa ngoma katika bendi za Congo kama vile  Viva la Musica ya Julius Wemba diuoshungu maarufu kama Papa wemba, Stukas, Nouvelle Generation na Loketo inayoongozwa na Arlus Mabere.
Mwaka wa 1995, Awilo aliamua kuachana na kazi aliyokuwa akiifanya ya kupiga Ngoma(Drum Boy) na badala yake akuamua kuimba. Alifanikiwa kutimia azima yake,kwani mwaka huo huo alitoa albamu yake ya kwanza iliyoitwa Moto Pamba, akipata kutoka kwa watu kama akina  Shimita El Diego, Ballou Canta, Dindo Yogo, Dally Kimoko, Sam Mangwana, Syran Mbenza na Rigo Star.
Album yake ya pili,iliitwa Coupe Bibamba ambayo aliitoa mwaka 1998. Na hii ndio iliyomtamburisha katika anga ya Muziki  kote barani Afrika, Ulaya na Amerika. Hii ilifuatiwa na Kafou Kafou mwaka wa 2001 na albamu yake ya hivi karibuni, Mondongo mwaka wa 2004, ambayo inawashirikisha Japponais, Dally Kimoko, Caen Madoka, Djudjuchet, Josky Kiambukta na Simaro Lutumba. Pia alishirikishwa kama atalaku (mtu wa kutumbuiza) katika baadhi ya rekodi za soukous.
Awilo kwa sasa anaishi nchini Ufaransa na inasemekana ana uhusiano wa kimapenzi na mwanamuziki Barbara Kanam.
Ndugu zake wengine katika sanaa muziki ni pamoja na baba yake Victor Longomba mwanachamana  mwanzilishi wa TP OK Jazz na vilevile Longombas ambalo ni kundi maarufu la afro-fusion lenye makao nchini Kenya.
Mnamo mwaka wa 2008 Awilo Longomba alitoa albamu nyinginealiyoiita  SUPER-MAN, ambayo ilikuwa na mafanikio makubwa. Umaarufu wake sio tu katika Bara la Afrika bali hata Marekani / na kanada ambako amefanikiwa kufanya matamasha ya kutangaza Album yake hiyo.

Na: Juventus Juvenary. Kwa Msaada wa internet

No comments:

Post a Comment