February 19, 2013

CHADEMA-WAZIRI WA ELIMU AJIUZURU

Kutokana na matokeo mabaya ya Mtihani wa kidato cha nne uliofanyika mwka jana, Chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA  kimetishia kufanya maandamano makubwa Nchini kushinikiza waziri wa elimu Shukuru Kawambwa na naibu wake kujiuzuru ikiwa hawatajiiuzuru kwa hiari ndani ya wiki mbili februari 19 mwaka huu
Bw. Mbowe amesema matokeo mabaya ya Mitihani yanatokana na usimamizi mbovu wa viongozi husika katika wizara ya elimu, na kwamba namna pekee ya kuwawajibisha ni kushinikiza wajiuzuru.                   

Katika hatua nyingine Mwenyekiti huyo wa CHADEMA amelaani vikali  matukio ya uvunjifu wa amani yanayotokana na Vurugu za kidini huku kikiyaita msiba kwa Taifa na adui mgeni anayeathiri maendeleo ya wananchi  huku kikiwatahadharisha viongozi wake kujiepusha  na matukio hayo

Bw. Mbowe amesema Serikali imeshindwa kudhibiti matukio hayo yanayoendelea kujitokeza hapa Nchini akitolea mfano matukio yaliyojitokeza hivi karibuni ya Buseresere mkoani Geita  na huko Zanzibar ambapo Padre wa kanisa katoliki aliuawa kwa kupigwa risasi na Kanisa kuchomwa moto
Aidha amesema viongozi wa CHADEMA watakaojihusisha na Vurugu hizo hawatavumiliwa.                   
Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA Freeman mbowe akiingia ndani ya ukumbi wa ASPEN jijini Mwanza kuzungumza na viongozi wa chama hicho kanda ya ziwa magharibi inayohusisha mikoa ya Mwanza Kagera na Geita
Wananchi waliokuwa katika mkutano wa hadhara wa CHADEMA katika uwanja wa FURAHISHA wakinyoosha mikono kama sehemu ya kuunga mkono tangazo la CHADEMA kuandamana kushinikiza Waziri wa elumu shukuru Kawamba kujiuzuru kufuatia matokeo mabaya ya kidato cha nne


Wafuasi wa Chadema wakiandamana mjini Mwanza

Wanachama wa CHADEMA wakisikitishwa na matokeo ya kidato cha nne

Wakimsikiliza freeman mbowe katika mkutano

kutoka kulia ni mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya biharamulo Bw. George Kasaize,Mbunge viti maalum na katibu wa CHADEMA Mkoa wa Kagera Bi. Concesta Rwamulaza,Mbunge wa Biharamulo Magharibi na Waziri kivuli wa wizara ya afya na ustawi wa jamii Dr. Anthony Gervase mbasa ba prof. Kulikoyera kanaruanda Kahigi mbunge wa Bukombe

                

No comments:

Post a Comment