February 4, 2013

MAADHIMISHO YA MIAKA 36 YA CCM

Picha kwa hisani ya Mdau Prosper Kwigize akiwa lake Tanganyika Kigoma-STANDARD RADIO FM-TANZANIAWAKATI MAADHIMISHO HAYO YAKIFANYIKA WILAYANI BIHARAMULO:-
Chama cha Mapinduzi CCM kimewataka wanachama na wafuasi wake kutumia siku ya maadhimisho ya miaka 36 tangu kuanzishwa kwa chama hicho kufanya tathimini ya mafanikio na kuweka mikakati ya kukiboresha kwaajili ya maendeleo ya wananchi

Wito huo umetolewa na Katibu wa CCM wilayani humo Bi. Odilia Francis Maholero wakati akizungumza na radio Kwizera Mjini Biharamulo

Bi. Maholero amesema maandalizi ya sherehe za maadhimisho ya siku ya kuzaliwa kwa CCM yanaendelea vizuri ambapo wilayani humo,sherehe hizo kiwilaya zitafanyika katika kata ya Kabindi
Hata hivyo maadhimisho hayo wilayani humo,yamefanyika Februari 4 wakati kilele kikiadhimishwa  Februari 5, ikiwa ni miaka 36 tangu Chama hicho kilipozaliwa Februari 5 mwaka 1977

Kwa upande wake mwenyekiti wa chama hicho wilaya ya Biharamulo Bw. Dominick Kasigwa amesema wanachama wa CCM wakienzi chama chao kwa kufanya kazi hasa kutekeleza miradi mbali mbali ya maendeleo katika jamii, hali itakayoepusha malalamiko kwa jamii kuwa serikali imewatelekeza
Katika hatua nyingine,ametoa wito kwa wananchi kuwa na mwamko wa kuhudhuria vikao na mikutano mbali mbali ya hadhara ambayo ndiko chimbuko la maendeleo,hasa pale jamii inapotakiwa kubuni na kuibua miradi ya maendeleo
Mgeni rasmi katika shughuli hiyo alikuwa Mkuu wa wilaya  hiyo Bw. Lichard Mbeho ambaye katika hotuba yake amewaka wananchi kuacha malumbano ya kisiasa hasa itikadi za vyama vingi badala yake waelekeze nguvu katika kufanya kazi.     


 Je,huko uliko wewe,maadhimisho hayo yalikuwaje? Tuma picha,habari na matukio hapa. www.juveilla@gmail.com

No comments:

Post a Comment