July 29, 2013

Jamii yatakiwa kuchangia watoto yatimaMganga mkuu wa Hospitali teule ya wilaya ya Biharamulo Mkoani Kagera amekabidhi Kilo 250 za Mchele kwa kituo cha kulelea watoto yatima MALAIKA kilichopo Rulenge wilayani Ngara kwaajili ya chakula cha watoto wanaolelewa kituoni hapo

Akikabidhi msaada huo,Dr. Gresmus Ssebuyoya amesema msaada huo umetokana na ahadi yake mwenyewe na uongozi wa hospitali teule ya Biharamulo huku akiwataka wanajamii wengine kujitolea kuwasaidia

Amesema,Uongozi wa Hospitali umetoa kilo 150,huku yeye binafsi akitoa Kilo 100 kwaajili ya kupunguza changamoto za chakula zinazokikabili kituo hicho
Dr.Gresmus Ssebuyoya akizungumza akizungumza na Juventus Juvenary wa ngarakwetu.blogspot.com

Dr.Gresmus Ssebuyoya

Dr.Gresmus Ssebuyoya akiwa na Sr. Mektilda Felecian na watoto wanaolelewa katika Kituo hichoMagunia ya Mchele


No comments:

Post a Comment