July 1, 2014

WANAHABARI WA KIGOMA WAFANYA UTALII WANDANI ARUSHA NATIONAL PARK

Mwanahabari wetu Mwemezi Muhingo ni mmoja wa wanahabari waliokuwa katika ziara hiyo ya takribani siku 8 ambaye amefanikisha kupatikana kwa picha za wanyama mbali mbali kama vivutio vya watalii na habari.
Tembo
Mmoja wa wahifadhi akitoa maelezo kwa wanahabari
Kundi la Pundamilia katika mbuga
Nyati
Wanahabari katika Picha
Mwemezi Muhingo Arusha

Baadhi ya Wananchi wa kijiji cha Ngarenanyuki wilayani Arumeru, Mkoa wa
Arusha, wameupongeza uongozi wa Hifadhi ya Taifa ya Arusha kwa huduma wanazozipata kutokana na Hifadhi hiyo,

Hayo yamesemwa na wakazi hao wanaoishi kwa kwenye vijiji ambavyo vinaizunguka hifadhi hiyo, wakati wa ziara ya waandishi wa habari wa mkoa wa Kigoma walipotembelea na kuona baadhi ya kazi zinazofanyika humo.

Wakazi hao wamesema kuwa kushirikiana na huongozi wamekuwa wakipatiwa ajira ndogondo za mara kwa mara ambazo zinawasaidia kuongeza pato katika familia zao ikiwa ni pamoja na kuwasindikiza watalii wakati wa kupanda mlima Meru ikiwa ni pamoja na   na kujengewa shule katika maeneo ya vijiji vyao na huduma za Afya zinazopatika hifadhini.


Pamoja na faida wanazozipata wametaja changamoto wanazokabiliana nazo kuwa ni wanyama kutoka ndani ya hifadhi na kushambulia mazao yao mashambani hali inayorudisha nyuma maendeleo katika shughuli za kilimo.


Hata hivyo mkuu  wa Idara ya Ujirani mwema wa Hifadhi ya Taifa ya Arusha, Bw, Nathanael Shafuni, amesema kuwa Idara yake na Hifadhi kwa ujumla, inakabiliana na changamoto mbalimbali kutoka kwa wakzi hao ambao wanaishi karibu kuwa kutafuta kuni za kupikia na kutaka kitoeo hali ambayo ni kinyume na taratibu lakini wanajitaidi kutoa elimu.ili waweze kuelewa na kuithamini hifadhi

Aidha amesema kuwa wamekuwa wakitoa elimu kwa wananchi hao waweze kuithamini hifadhi na kujua kuwa ni mali yao na na Taifa kwa ujumla hatua iliyopelekea kuwashirikisha katika shughuli mbalimbali za kufanya ili kujiongezea kipato cha familia

Kwa upande wake mkuu wa Hifadhi hiyo Bi, Maria Kilombo wamewataka Watanzania kuendelea kujijengea tabia ya kufanya utalii wa ndani katika za Hifadhi zilizopo hapa nchini na kuondoa tabia ya kusema kuwa hiyo ni kazi ya wazungu kwani hata wao ni yao na wanaongeza pato la Taifa na kutaja idadi ya watalii wandani kufikia mwaka 2012/2013


Nae kaimu  mkuu wa Idara ya Utalii Bwa,Samusa Kinoih, amsema kuwa wamekuwa wakiwahamasisha watalii wa ndani ili kuwazoesha kufanya utalii


Mwisho

No comments:

Post a Comment