February 13, 2015

TAARIFA ZA MAENDELEO YA KATA BARAZA LA MADIWANI NGARA

Ni Bahati sana kuwepo nyumbani na nikapata taarifa kuwa kuna Kikao cha baraza la Madiwani Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Mwenyekiti wa Halmashauri ni Diwani wa kata yangu Mh.John Shimlmana

Katika taarifa yake,Mh. John Shimilmana ameeleza kuwa Wanafunzi 80 pekee ndio wameripoti kuanza masomoya shule ya Sekondari Kibimba kati ya wanafunzi 109 waliochaguliwa kujiunga na masomo ya Sekondari katika shule hiyo

Bw.Shimilimana amesema kati ya wanafunzi hao waliojiunga na shule za sekondarinza binafsi ni 12

Aidha kutokana na utoro huo,ameeleza kuwa uongozi wa kata umeagiza wazazi na walezi ambao watoto wao hawajaripoti kufika ofisini kwaajiki ya kutoa taarifa na kwamba watakaokiuka watachukuliwa hatua.
Mwenyekiti wa Halmashauri wilaya ya Ngara na diwani wa kata ya kibimba Mh.John Shimlimana akifunga kikao cha baraza la madiwani

Madiwani wakifuatilia Kikao

Waheshimiwa Madiwani wakisoma taarifa

No comments:

Post a Comment