Zaidi
ya kaya masikini zipatazo 100 katika Kijiji cha Buhororo wilayani Ngara
mkoani Kagera zinatarajia Kuanza kupata Ruzuku kutoka Mfuko wa hifadhi ya jamii
TASAF awamu ya tatu ikiwa na lengo la kunusuru kaya masikini
Hali
hiyo inatokana na hatua za awali za kutamb ua na kubaini kaya hizo katika zoezi
lililofanyika hivi karibuni kijijini humo na kubarikiwa na Vikao vya
halmashauri ya kijiji pamoja na mkutano mkuu wa wananchi
Mmoja wa maafisa kutoka TASAF Dk. Richard
Ngowi amesema ruzuku zitatolewa kulingana na mahitaji ya kaya husika na kwamba
zimegawanyika katika makundi mawili ambayo ni Ruzuku muhimu na ruzuku ya
masharti
Katika
vikao vya awali ,afisa mwingine wa TASAF Bi. Hellen Mkongwa amewataka walengwa
kuhakikisha ruzuku zitakazotolewa zinatumika ipasavyo ili kufikia malengo.
Dkt. Richard Ngowi akitamburisha Mradi katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika katika viwanja vya Zahanati ya Buhororo |
Baadhi ya Vijana wakifuatilia Mkutano |
Mmoja wa wananchi akiuliza Swali |
Akina mama wakisikiliza kwa makini maelezo juu ya Mradi |
No comments:
Post a Comment