November 11, 2015

SOKO LA WAKULIMA KAHAMA ,WATUMIAJI WAHOFIA KIPINDU PINDU

www.ngarakwetu.blogspot.com iko mjini Kahama katika Soko la wakulima,hali inayoonekana hapa ni kukithiri kwa uchafu!!!!!!!! hali inayohatarisha maisha ya watumiaji.    Juventus Juvenary kama mwanahabari anayefanya kazi na Radio Kwizera ameandika habari.KAHAMA

Baadhi ya wakazi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama mkoani Shinyanga wanaotegemea huduma kutoka katika Soko la wakulima Mjini Kahama wameeleza kuwa hali zao kiafya ziko mashakani kutokana na kukithiri kwa uchafu
Hayo yameelezwa na wananchi hao wakati wakizungumza na Radio Kwizera sokoni hapo

Mmoja  wa wafanya biashara wa Mboga za majani katika soko hilo Bi.Paskazia Elias amesema hali ya uchafu wa soko hilo unahatarisha maisha yao,huku mfanya biashara wa kuku Bw.Adidas Gideon akiitaka Srikali kuongeza hamasa kwa uongozi wa soko kuhusu usafi
Insert:-wafanya Biashara


Kutokana na hali hiyo,Afisa afya wa mji wa Kahama Bw.Deogratis Simon Dotto ametoa wito kwa wafanya Biashara sokoni humo kuzingatia masharti ya afya kwa kufanya usafi huku akisema kuwa watakaokiuka watachukuliwa hatua.    EndS

Juventus Juvenary akizungumza na mmoja wawafanyabiashara katika soko la wakulima mjini Kahama Bi Paschazia Elias

Kutoka kushoto ni Mwanahabari Simon Dionizy akirekodi sauti ya mfanya biashara,aliyesimama ni Juventus Juvenary-ngarakwetu.blogspot.com


Uchafu sokoni


Juventus

Juventus akielekea Sokoni 

Simon Dionizy akifanya mahojiano na mfanya Biashara sokoni kuhusu hali ya usafi

Hali ni ya hatari! Jitihada za maksudi zinatakiwa kuchukuliwa ili kunusuru afya za wananchi.   
mahojiano na wafanya biashara wengine


Mawe kwaajili ya ujenzi wa miundombinu sokoni

Moja ya maduka ya nyama sokoni hapo. Idara ya Afya  Katika Halmashauri ya mji imetoa notisi ya siku 90 kwa wamiliki wa maduka hayo kuhakikisha wanaboresha huduma kuepuka kufungiwa
Picha na Emmanuel Mlelekwa-ngarakwetu.blogspot.com

No comments:

Post a Comment