December 22, 2015

RADIO KWIZERA SASA KUSIKIKA KAHAMA

RADIO KWIZERA INAENDELEA KUPANUA WIGO WA USIKIVU,SASA WAKAZI WA KAHAMA-SHINYANGA WATAANZA KUPATA MATANGAZO YA MOJA KWA MOJA.

Hatua za Ujenzi zinaelekea kukamilika.

Na Juventus Juvenary-Radio Kwizera-Kahama.

Tarehe 4.11.2015, nilitaarifiwa rasmi na mkurugenzi wa radio Kwizera kuwa nahamishiwa Kahama kama Ripota. NiliRipoti katika kituo cha kazi tarehe 6.11.2015 na kuanza kazi rasmi kesho yake ikiwa ni Tarehe 7. Ushirikiano Mkubwa sana niliupata kutoka kwa Mwanahabari mwenzangu Simon Dionizy pamoja na wanahabari wengine wanaofanya kazi na Vyombo mbali mbali hapa Wilayani Kahama na Mkoa wa Shinyanga kwa ujumla

Mbali na majukumu ya Kihabari,Ujenzi wa Mnara na Ofisi Mjini Kahama ndio hasa Jambo linaowagusa watu ninaokutana nao,ninaofahamiana nao, na watu wanaotaka kupata habari hasa kutoka Radio Kwizera yenye miaka 20 tangu ianze kutoa Huduma.
Pichani:-Mimi Juventus Juvenary nikitoka Nyumbani n inakoishi-Kahama kuelekea kwenye majukumu ya kutafuta habari,bila kusahau kupita eneo unakojengwa mnara wa Radio Kwizera Igalilimi mlimani juu ya Polis

Mnara

Nikifanya mawasiliano Mnarani


Ujenzi wa ukuta wa jengo la Mashine(TX Room)


Ujenzi unaendelea

No comments:

Post a Comment