December 18, 2015

Muasisi Jimbo Katoliki -Kahama Askofu Matheo Shija azikwa

Pichani,Maaskofu Kutoka majimbo mbali mbali Katika Kanisa la Mt. Karoli Lwanga jimbo kuu la Kahama,Ibaada maalum ya mazishi ya aliyekuwa Askofu mkuu wa jimbo hilo Matheo Shija aliyefariki Desemba 9,2015
KUKUMBUKA
Alizaliwa April 17 mnamo 1924
Amefariki Desemba 9, 2015
Mazishi yake yamefanyika Desemba 17,2015
HABARI: Juventus Juvenary,Kahama
Rais wa baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania Mhashamu Askofu Taracisis Ngaralekumtwa amewataka waumini wa Jimbo Katoliki kahama kumuenzi aliyekuwa Muasisi wa jimbo hilo kwakufanya kazi kwa bidii na kuimarisha mshikamano

Askofu Ngaralekumtwa ametoa rai hiyo wakati wa Ibaada ya mazishi ya hayati Askofu Matheo Shija aliyefariki dunia Disemba 9 mwaka huu baada ya kuanguka ghafla mbele ya nyumba aliyokuwa akiishi

Katika ibaada hiyo iliyofanyika kwenye kanisa kuu la Mtakatifu Karoli Lwanga mjini Kahama,rais huyo wa Baraza la Maaskofu wa Katoliki amesema Hayati Askofu Matheo Shija alikuwa na mchango mkubwa katika kanisa kwa kuziishi TUNU zilizolenga kuendelea mshikamano Nchini

Akitoa salaam za rambi rambi kutoka Kwa kiongozi wa dhehebu la Kikatoliki Duniani Papa Francis katika Ujumbe wake uliowasilishwa na Barozi wake hapa NchiniAskofu Mkuu Francisco Pardilla amesema baba Mtakatifu anaungana na waumini wa Jimbo la Kahama katika kipindi hiki cha huzuni na kuwataka kuenzi matendo mema aliyoyaasisi.       
Mazishi ya askofu Shija yalihudhuriwa na viongozi mbali mbali wa kidini,Vyama na Serikali kutoka sehemu mbali mbali, ambapo katika salaam za rambi rambi kutoka baraza la Maaskofu wa Katoliki zilizowasilishwa na rais wa Baraza hilo Mhashamu Askofu Taracisis Ngaralekumtwa amewataka waumini wa Jimbo Katoliki kahama kumuenzi askofu Shija  kwakufanya kazi kwa bidii na kuimarisha mshikamano

Naye Balozi wa Papa hapa Nchini Askofu Mkuu Franchesco  Pardilla kakatoa salaam za rambi rambi zikiambatana na ujumbe kutoka kwa kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani Baba Mtakatifu Papa Francis

Awali ilitegemewa kuwa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli angeshiriki katika maziko hayo,lakini taarifa zilizotolewa na mmoja wa wasemaji zikaeleza kuwa ametoa taarifa za kutofanikiwa huku akiwatakia Pole waumini ndugu jamaa na Viongozi wa dini

Licha ya sifa kemkem zilizotolewa kwa hayati Askofu Shijja,Mkuu wa wilaya ya kahama Vitta Kawawa akamtaja kuwa alikuwa kiungo kikubwa kufanikisha maendeleo na ustawi wa wilaya hiyo,na mchango mkubwa kwa Serikali kutokana na kuwa alikuwa akiwasaidia wafungwa kwa huduma mbali mbali

Hayati ASkofu Matheo Shijja ambaye katika Uhai wake alipenda kuitumia kaulimbiu ya “MUNGU ANA SAA YAKE”,alizaliwa 17/04/1924 huko Puge Tabora,na amezikwa 17/12/2015 Jimboni Kahama.  

No comments:

Post a Comment