February 19, 2016

WAWILI WAFA,WAKICHIMBA DHAHABU-KAHAMA

                    WAWILI WAFA,WAKICHIMBA DHAHABU-KAHAMA

KIFUSI CHA DHAHABU CHA UA WACHIMBAJI-KAHAMA

WATU wawili wamethibitika kupoteza maisha baada ya kufukiwa na kifusi katika machimbo madogo ya madini ya Dhahabu Mwanziro yaliyoko katika Kijiji cha Isalange kata ya Iyenze wilayani Kahama Mkoani Shinyanga.
Licha ya kuwa taarifa za vifo hivyo zimeanza kujulikana kwa kuchelewa, vyanzo vinaeleza kuwa ni kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ni Maamuzi ya kutofukuliwa na kuopoa miili ya marehemu yalifikiwa na Kamati ya ulinzi na usalama baada ya kupewa taarifa na kuridhia hivo.
Hata hivyo,baada ya kupatikana kwa taarifa hizo Mkuu wa wilaya hiyo Vitta Kawawa alisema  hana taarifa hizo na kuwataka wanahabari kufuatilia kwa afisa madini wilaya.
Alipofuatwa ofisini kwake,afisa madini wilayani humo Bi.Sofia Omary alikataa kuzungumza nakuwataka waandishi wa habari wasimrekodi huku akisema kuwa kuna mtu maalum aliyemteuwa na kulizungumzia bila kusema ni lini mtu huyo ataliongelea.
Baada ya mkwamo huo,jitihada zikafanyika kumtafuta Kamishina msaidizi wa Madini  anayeshughulikia ukaguzi wa migodi hapa Nchini Mhandisi  Ally Samaje ambaye alikiri kupewa taarifa hizo na kueleza kuwa tukio hilo lilitokea Januari 16 mwaka huu ambapo waliofukiwa walikuwa wachimbaji wasio rasmi na kwamba walikuwa wakichimba kwakuiba maarufu kama (manyani).  
Baada ya taarifa hizo kusambaa katika maeneo mbali mbali ya wilaya ya Kahama, wananchi  Wameilalamikia Serikali kwakushindwa kufanyan jitihada za maksudi kuopoa mili ya wahanga wa tukio hilo.
Mmoja wa wananchi hao Rajab Habib alisema kuwa kama serikali ingekuwa makini watu hao wangeopolewa na kuchukuliwa na ndugu zao kwenda kuzikwa majumbani kwao tofauti na maamuzi yaliyofikiwa na Kamati ya Ulinzi na usalama kufukia shimo walilokuwemo wachimbaji hao na kulifanya kuwa kaburi la pamoja.

Mmoja wa wachimbaji ambaye alisema kuwa muda mfupi kabla ya tukio hilo kutokea amesema kama Serikali ingelichukulia maanani suala hilo kulikuwa na uwezekano wa kutoa maiti kwakuwa hata baada ya kufukiwa walijaribu kuwafukua na walipowafikia wakakutana na mwamba wa dhahabu wakaanza kuchiba na kubeba mawe huku wakiiacha miili hiyo.
Alisema baada ya watu hao kuondoa dhahabu,ghafla shimo lilititia kwa mara nyingine na kuwafukia marehemu hali iliyopelekea shughuli ya kuwachimba na kuwatoa kuwa ngumu zaidi lakini kama Serikali ikiamua hata leo inaweza kuwatoa.
Mwananchi mwingine aliyejitamburisha kwa jina la Peace alisema Serikali bado inanafasi ya kulishughulikia suala hilo kwakuomba msaada kutoka kjatika Kampuni ya ACACIA inayosimamia Mgodi wa dhahabu Buzwagi ambayo ina vifaa vyenye uwezo wa kufukua na kuiopoa miili ya marehemu.

Aidha,mmoja wa wachimbaji katika mgodi wa Isalange yalikotokea mauaji hayo alisema takwimu inayotajwa ya watu wawili kuwa ndio waliofariki si ya kweli bali ndani yua duala moja walikuwa watu  watanoa ambapo alitoka peke yake hivyo wengine wane walifukiwa.
Akizungumzia tukio hilo,Mkurugenzi wa umoja wa wachimbaji katika mgodi huo Waziri John alikanusha taarifa za idadi ya watu zaidi ya wawili kupteza maisha huku akisisitiza kuwa kabla ya kufukiwa walikuwa watatu na mmoja alifanikiwa kutoka
Hata hivyo,wananchi waliozungumzia maafa hayo wameitaka serikali kutengua azimio la kubariki kaburi la pmoja kwa kigezo cha ugumu wa kuwafukua watu hao badala yake itafute msaada wa Vifaa kutoka katika Mgodi wa Buzwagi ili kujiridhisha na idadi hiyo.   Mwisho.

No comments:

Post a Comment