March 1, 2016

Mujuru abuni chama kumpinga Mugabe


Aliyekuwa mwandani wa rais wa Zimbabwe Robert Mugabe amezindua chama chake kitakachompinga rais huyo.
Joice Mujuru amesema kuwa chama cha Zimbabwe Peoples party ZPF kilibuniwa kwa sababu Zimbabwe ni taifa lililogawanyika.
Bi Mujuru alikuwa wa pili kwa ukubwa hadi chama tawala cha Zanu-PF kilipomfuta kazi mwaka 2014 baada ya kumshtumu kwa kupanga njama za kumuondoa na kumuua Mugabe.
Mimi sio muuaji wala mchawi,bi Mujuru alisema wakati wa uzinduzi wa chama hicho katika mji mkuu wa Harare.
Ni afisa mkuu wa ngazi za juu katika chama cha Zanu-PF kubuni chama cha upinzani na anatarajiwa kuwa mgombea wake wa urais mwaka 2018.
Wafuasi wake walipiga vigelegele alipoingia katika ukumbi huo ili kuzindua chama hicho,alisema mwandishi wa BBC Nomsa Maseko kutoka eneo hilo.
Bi Mujuru aliandamana na wanachama wengine wa zamani wa ZANU-PF akiwemo Diymus Mutasa na Rukare Gumbo.

No comments:

Post a Comment