June 8, 2016

BAJETI YA TANZANIA 2016 / 2017


Naam msomaji na mfuatiliaji wa blogu hii,  makadirio ya bajeti ya mwaka 2016 na 2017 hapa nchini ni trilioni 29,5 pesa za Tanzania ikiizidi bajeti ya mwaka wa 2015 na 2016 kwa trilioni 7.1.
Waziri wa Fedha hapa nchini Tanzania Phillip Mpango alisema kuwa kati ya fedha hizo, Shilingi trilioni 18.46 zitatokana na jumla ya mapato ya ndani.
Kiwango hicho kimezidi shilingi trilioni 3.64 za bajeti iliyopita ambayo ililenga kukusanya shilingi trilioni 4.82.
Shilingi trilioni 17.72 zitakuwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida, huku trilioni 11.82 sawa na asilimia 40 ya bajeti nzima, zikitengwa kwa ajili ya shughuli za maendeleo.
Bwana Mpango alisema washirika wa maendeleo wanatarajiwa kuchangia shilingi trilioni 3.6, ikiwa ni ongezeko la shilingi trilioni 1.7 ikilinganishwa na shilingi trilioni 1.88 zilizokuwa zinategemewa kwenye bajeti iliyopita.
                                      www.ngarakwetu.blogspot.com

No comments:

Post a Comment