WANANCHI WALALAMIKIA MATUMIZI YA NGUVU YA POLIS KUTAWANYA MAAANDAMANO.
Gari la Jeshi la Polis likipita mtaani kuwatangazia wananchi kuhusu zuio la Mkutano.
Gari la maji yanayowasha |
Baadhi ya wananchi wilayani Kahama Mkoani
Shinyanga wamelalamikia matumizi ya nguvu za jeshi la Polis mkoani humo
zilizotumika kuwatawanya wafuasi wa Chama Cha demokrasia na maendeleo CHADEMA
waliokuwa katika mkutano wakidai kuwa matumizi ya nguvu yamewaathiri wananchi
wasio na hatia
Wananchi hao wameeleza hayo kufuatia
kitendo Jeshi hilo kutumia Mambomu ya Mchozi na maji ya kuwasha kuwatawanya
watu waliokuwa katika Mkutano uliokuwa umepangwa kufanyika June 7 mwaka huu
katika Uwanja wa CDT Mjini Kahama
Baadhi ya wananchi hao Alfred Festo,Yona
Masabile na Augenia Masabo wamesema kuwa kitendo cha jeshi hilo kutumia nguvu
kubwa kwa wananchi ni ukiukwaji wa haki za Binadamu na Vurugu kwakuwa wananchi
waliokuwa katika Mkutano hawakuwa na fujo wala silaha
Hayo yameelezwa ikiwa ni siku moja baada
ya Jeshi la Polis wilayani Kahama kwakushirikiana na askari wa jeshi hilo
kutoka Mkoani kulipua mabomu ya kutoa machozi,kuwamwagia wananchi maji ya
kuwasha na kuwasulubu baadhi ya wananchi waliokuwa Mkutanoni.
www.ngarakwetu.blogspot.com
No comments:
Post a Comment