June 27, 2016

LALA MAHALI PEMA KAMANDA MBASSA

www.ngarakwetu.blogspot.com, inaungana na Familia ya Dkt.Anthony Gervase Mbassa katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo ya Msiba wa ndugu yetu,Mpendwa wetu Dkt.Anthony Gervase Mbassa aliyetutoka June 26,2016.

Hakika napata ugumu wa ainagani ya neno/maneno ya kutumia hasa ili uelewe ni kwa namna gani Msiba huu umetugusa!

Tangulia Kamanda,mbele yetu,nyuma yako. Pumzika kwa amani.
Dkt.Anthony Gervase Mbassa,aliwahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Biharamulo Magharibi2010-2015. Alikuwa pia Daktari katika Hospitali teule ya Wilaya ya Biharamulo.

No comments:

Post a Comment