June 28, 2016

HIFADHI KUBWA YA GESI NCHINI TANZANIA.


Ni rahisi kwa mtu anayejua kujiuliza Tanzania tuna Bahati gani na Rasilimali? Je,manufaa yake yako wazi na Watanzania wanatambua?


Taarifa katika Vyombo mbali mbali vya habari zimesambaa kuhusu uwepo wa rasirimali gesi hapa Nchini.Hii nimeitoa http://www.bbc.com/swahili

Tanzania ni miongoni mwa mataifa chache duniani yaliyojaliwa kuwa na rasilimali na madini mengi.
Na baada ya kugunduliwa kwa gesi asili huko Mtwara na dhahabu sasa watafiti kutoka Uingereza wamegundua hifadhi kubwa zaidi duniani ya gesi adimu zaidi ya Helium nchini Tanzania.
Watafiti kutoka chuo kikuu cha Oxford na kile cha Durham kwa ushirikiano na wataalumu wa madini kutoka Norway wamegundua uwepo wa takriban futi bilioni 54 za gesi hiyo ya barafu kama inavyofahamika.
Ugunduzi huo umefanyika katika eneo la bonde la ufa la Tanzania.
Katika taarifa kwa wanahabri huko Japan, watafiti hao wanasema kuwa uhaba wa gesi hiyo kote duniani ulikuwa umesababisha taharuki haswa kwa madaktari ambao wanatumia gesi hiyo adimu kuendesha mashine za utabibu zijulikanazo kama MRI scanners, mbali na kutumika katika mitambo ya kinyuklia miongoni mwa sekta zingine nyingi za kawi na teknolojia.
Kabla ugunduzi huo watafiti walikuwa wamebashiri ukosefu wa gesi hiyo baridi ifikapo mwaka wa 2035.
Mnamo mwaka wa 2010 Mwanfisikia mshindi wa tuzo la Nobel Robert Richardson alikuwa ametabiri kumalizika kabisa kwa gesi hiyo.
Ukosefu huo ulikuwa umesababisha wataalamu kuhimiza kutungwa kwa sheria itakayopunguza matumizi yake katika bidhaa zisizo za dharura kama vile kwenye vibofu kutokana na hali ya kuwa gesi hiyo ya Helium ni nyepesi kuliko ile ya Oxygen.
''Gesi tuliyoipata huko Tanzania inaweza kujaza silinda za gesi milioni moja nukta mbili za mashine za MRI'' alisema Chris Ballentine kutoka chuo kikuu cha Oxford.
MUNGU IBARIKI TANZANIA,BARIKI WATANZANIA NA TUPE UTASHI WA MATUMIZI MEMA YA RASIRIMALI KWA MAENDELEO.

www.ngarakwetu.blogspot.com

No comments:

Post a Comment