June 18, 2016

MITANDAO YA KIJAMII YAPUNGUKIWA WATEJA,BAADA YA SIMU KUZIMWA TANZANIA.


Imenichukua muda kujua kuwa chanzo ni TCRA kuzima Simu za wananchi!

Maelfu ya Watanzania hawawezi kuwasiliana na rafiki zao, familia zao ama hata kupiga simu za kibiashara kupitia simu zao za mkononi.
Hii ni kwa sababu usiku wa kuamkia Ijumaa  tarehe 17,07,2016 serikali  kupitia mamlaka husika ya matangazo na mawasiliano ilizima simu zote bandia.
Tanzania inaungana na nchi nyingine barani humo zikiwemo Cameroon, Kenya na Nigeria katika hatua ya kuziondoa kabisa simu bandia nchini.
Hata hivyo,baadhi ya wananchi wamelalamikia kitendo hicho kuwa Simu walizonunua hawakujua kama ni bandia au la! na lawama nyingine zinaigeukia Serikali kupitia mamlaka zinazohusika na uidhinishaji wa vifaa au bidhaa zinazoingizwa nchini kutoka Nje.
Baadhi ya wapenzi na wafuatiliaji wa mitandao ya Kijamii sasa hawana namna ya kuingia kufanya shughuli zao yakiwemo mawasiliano .
www.ngarakwetu.blogspot.com

No comments:

Post a Comment