June 17, 2016

TZ yataka uzoefu wa Qatar sekta ya gesi


Rais Magufuli na balozi wa Qatar nchini Tanzania bwana Abdallah Jassim Al Maadadi. 
Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa taifa lake linakusudia kufanya biashara na jamhuri ya Qatar haswa katika sekta ya gesi na usafiri wa ndege.
Rais Magufuli aliyasema hayo baada ya kukutana na balozi wa Qatar nchini Tanzania bwana Abdallah Jassim Al Maadadi.
Aidha rais Magufuli alitangaza nia ya kufungua ubalozi wa Tanzania mjini Doha kwa lengo la ''kuendeleza na kuimarisha zaidi uhusiano na ushirikiano na taifa hilo tajiri la ghuba.
"Najua Qatar ina uzoefu katika maeneo hayo na sisi Tanzania tungependa tushirikiane nanyi kuwekeza na kubadilishana uzoefu ili fursa hizo zilete manufaa kwa pande zote mbili" amesema bw Magufuli.



www.ngarakwetu.blogspot.com

No comments:

Post a Comment