November 3, 2016

SHDEPHA+ WAHIMIZA WADAU,VYOMBO VYA HABARI KUKOMESHA UKATILI WA KIJINSIA-KAHAMA

Wilaya ya Kahama iliyoko Mkoani Shinyanga,imetajwa kuwa na Kiwango kikubwa cha Ukatili wa Kijinsia hasa kwa watoto kunyanyaswa,watoto wa Kike kubebeshwa Mimba na wanawake kubakwa na  kupigwa

Mkurugenzi wa Miradi ya SHDEPHA Kahama,Bw.Venance Muzuka akizungumza na Vyombo vya habari
 Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Shirika moja lisilo la Kiserikali SDEPHA +  Bw.Venance Mzuka wakati akizungumza na Vyombo vya habari Ofisini kwake Mjini Kahama

Bw.Mzuka amesema kwa watoto pekee Jumla ya watoto wa kike 21 katika shule mbalimbali za Sekondari katika Halmashauri ya mji wa Kahama wameripotiwa kubebeshwa mimba katika kipindi cha January hadi September mwaka huu

Mkurugenzi wa SHDEPHA Bw.Venance Muzuka(Kulia,) akizungumza na Vyombo vya habari, pembeni yake ni Bw.Kazungu Barnabas ambaye ni Msimamizi wa msimamiizi/anayeshughulikia masuala ya Wahanga wa ukatili
 Amesema Takwimu hizo ni matukio machache yaliyotolewa taaarifa kati ya mengi katika mkoa wa Shinyanga unaotajwa kuongoza kwa vitendo vya ukatili wa Kijinsia, takwimu za Halmashauri ya Mji wa kahama pekee kati ya Halmashauri 3 zinzounda wilaya hiyo

 Aidha mkurugenzi huyo amesema Shirika lake linatarajia kufanya maadhimisho ya ukatili wa kijinsia kuanzia Novemba 25 hadi Decemba 10 mwaka huu ambapo Katika kipindi hicho cha maadhimisho, wito umetolewa kwa wananchi wote hasa waliowahi kufanyiwa ukatili kujitokeza kwaajili ya kupatiwa huduma za upimaji wa afya, Ushauri wa kisheria na Saikolojia.
Kushoto ni Bi.Shekha Nassor ambaye ni Mratibu wa Mradi wa SAUTI ulioko chini ya SHDEPHA akiwa na Muelimishaji rika Bi.Edith Edward Mugerezi
 Kwa upande wake Bi.Shekha Nassor ambaye ni Mratibu wa Mradi wa SAUTI ulioko chini ya SHDEPHA,Matendo ya Ukatili wa Kijinsia katika wilaya ya kahama yanaendelea kushamili kutokana na wahanga kutojua vitendo wanavyofanyiwa kuwa ni Ukatili

Mkurugenzi wa SHDEPHA Bw.Venance Muzuka na Bi.Shekha Nassor ambaye ni Mratibu wa Mradi wa SAUTI
Naye, Muelimishaji rika wa shirika hilo Bi.Edith Edward Mugerezi amesema vitendo vya ykatili wa kijinsia vinaiweka jamii katika uduni wa maendeleo kwakuwa wahanga wengi huathirka kisaikolojia na wengine kupata maambukizi ya virusi vya UKIMWI.       EndS

            www.ngarakwetu.blogspot.com

No comments:

Post a Comment