October 24, 2012

BREAKING NEWS…



Watu watatu wanusurika kifo-Ngara
    Na.Shaaban Ndyamukama-ngarakwetublogspot.com
Watu 3 wamenususurika kupoteza maisha  baada ya gari walilokuwa wakisaifiria kupata ajali katika eneo la Murugarama wilayani Ngara mkoa wa kagera wakitoka Nchini Burundi kwenda jijini   Dar es salaam Tanzania
Ajali hiyo imetolkea Oktoba 23 kwa kulihusisha Gari aina ya Scania Semi teller lenye no. T949 ADR lenye trela no.T597 ABG mali ya Suleiman Suri mfanya biashara wa temeke jijini dare s Salaam
Akiongea na ngarakwetublogspot mmoja wa walionusurika katika ajali hiyo Muuba Mohamed mwenye umri wa miaka 39 amewataja wenzake waliojeruhiwa kuwa ni pamoja na driver Kassim Mussa 42 na Omary issa 34 wote wakazi wa Temeke jijini dare s salaam
Mohamed amesema gari hilo lilikuwa likikwepa shimo katikati ya barabara kutoka kabanga kwenda mjini Ngara, na kwamba gurudumu la nyuma lilitumbukia katika shimo hilo na kupelekea gari kuyumba ambapo dreva alishindindwa kumudu usukani wa  gari na Gari kupinduka ukingoni mwa barabara

Amesema majeruhi wote wamelazwa katika Hospitali teule ya Murgwanza na dreva Kassim Mussa alivunjika mkono na Omary Issa alijeruhiwa sehemu mbali mbali za Mwili wake

Amesema ajali hiyo ni ya pili kwa gari hilo kufuatia ajali nyingine iliyotokea Nchini Burundi wakati gari hilo likitoka dare s salaam. Jeshi la polisi lilithibitisha

Baadhi ya wakazi wa Murugarama wameiomba Serikali kupitia wakala wa barabara TANROADS  kufanya jitihada za kurekebisha eneo hilo kwani ni eneo korofi na kwamba ajali hiyo ni ya pili katika eneo hilo na kwamba baadhi ya watu wamepoteza maisha,uharibifu wa magari na maili


Mmoja wa wakazi wa Murugarama Bw Paul kabona amesema “ikiwa serikali inajali maisha ya watu kupitia usalama barabarani haina budi kuweka miundombinu bora, ikiwa ni pamoja na alama za barabarani na kudhibiti mwendo kasi wa madereva barabarani”

No comments:

Post a Comment