November 14, 2012

AKIWEZESHWA ANAWEZA KUMUDU MAISHA

Kainula AloysNa:-Shaaban Nassibu Ndyamukama
Katika kujiinua kimaisha Binadamu anahitaji kufanya kazi kwa kutumia akili na viungo vyake vya mwili ili kujikwamua kimaisha katika familia.
Watu walio wengi wamekuwa wakikosa kufanya kazi kwa kutumia maumbile yao kwa madai kazi hakuna wakitaka za  ofisini na kulipwa mishahara na serikali au mashirika yakiwemo makampuni.

Pia jamii imekuwa ikiwabeza walio na hitilafu za maumbile hasa walemavu wa viungo vya mwili kwa kukosa kuwasaidia katika kujiajiri na kupata riziki aidha mashirika ama taasisi binafsi na kuwafanya walio na mahitaji maalum kukosa mwelekeo wa maisha

 Suala hili limekuwa na mtazamo Tofauti kwa Baadhi ya walemavu kuwa kuwa nahitilafu za viungo si kuwa omba omba mitaani waweza kujishughulisha na kazi ndogo na hatimaye kujikwamua kwa kujiajiri na kupata kipato kinachosaidia kupata fedha nakujijengea  makazi bora ukisubiria serikali na taasisi nyinginezo kuongeza nguvu kwenye juhudi zako.

Hali hiyo nimeikuta kwa mjasiliamali mlemavu wilayani Muleba anayefanya kazi ya kushona viatu Muleba mjini Bw Aloyse Kainunula Pichani hapo juu aliyesema kuwa alipata ulemavu wa miguu akiwa mtoto baada ya kuugua polio na anatembelea kiuno lakini kwa kazi hiyo sasa ana mke na watoto watatu licha ya kwamba hakujaliwa kwenda shule ya aina yoyote.

Bw Kainunula hapati msaada wowote wa kijamii anaishi kwa nguvu na maombi ya kutaka walio na viatu viharibike ili waeze kuletea na kufanya ukarabati kwa kupata malipo ya shilingi 300 hadi 1000 kwa mteja na mtaji wake ni Matairi ya gari yaliyokwisha choka barabarani ili kuingiza sori na nyuzi za katani anazosokota kushonea viatu hivyo akikosa fedha za kununulia nyuzi za Nyloni.
Wasamalia wema kama mpo kazi yake anaifanyia ndani ya bandala magunia machakavu na makasha ya kufungia bidhaa yaliyochanika lakini akiwezeshwa sehemu nzuri ya kazi anaweza kuhimili mikiki ya maisha kwani bado ni mdogo ana umri wa miaka 35 tu Mashirika ya kidini yanayotoa msaada angalieni kiumbe huyo wa Mungu anayeishi Muleba mjini akiwakiwa na jua la mwaka mzima na kunyeshewa mvua ya mwaka mzima huku tuliojaliwa neema ya mungu tukipata na kusaza bila kumtole sadaka mungu kupitia kwa malio na mahitaji.

No comments:

Post a Comment