November 7, 2012

Habari kutoka kwa Mdau wa Misenyi[9:54:11 AM] Fidelis Camilius Kachinde: MISENYI

Baadhi ya wananchi wa eneo la mtukula wengi wao wakiwa kinamama wajasiriamali na vijana wamefanya vurugu katika eneo hilo la mpakani wakipinga kitendo cha kufungwa pingu mwenekiti wao, na kupitishwa kwa kila kibanda ili alipe fedha alizo watoza wananchi hao wakati akiwagawia meeneo ya mda ya kufanyia biashara.

Habari kutoka huko zinasema kuwa mwenyekiti huyo aliletwa na gari na serekali ya halmashauri ya wilaya hiyo kwa wananchi wake, ili kila mmoja ataje kile alicho kitoa kwa mwenyekiti, naye awarudishi hapo kwa hapo.

Hata hivyo hali ilibadilika baada ya wananchi kutaka mwenyekiti wao, waliomwita mpenda maendeleo aachiwe huru kwakufunguliwa pingu ndipo watakapo kubali kuongelea  swaala la kilicho tolewa na kupokelwa na mwenyekiti huyo, ambapo pia ilishindikana kuachiliwa na kurudishwa tena katika ofisi za halmashauri.

No comments:

Post a Comment