April 8, 2013

JIMBO LA BUKOBA LAPATA ASKOFU

Ni Askofu Desderius Rwoma aliyehama kutoka Singida.
Basi lililosafirisha watu kutoka Singida-Bukoba kumsindikiza askofu Desderius Rwoma

Gari lililokuwa katika Msfara


Kutoka Kushoto ni Mhasham Baba askofu Severin Niwemugizi akizungumza na Askofu Rwoma mbele ya kanisa Katoliki la Biharamulo,Baada ya Misa ya asubuhi kabla ya safari kuelekea Bukoba

Askofu Severin Niwemugizi akiwa na Askofu Rwoma-Biharamulo


Hapa ni Kanisa kuu la Bukoba

Maaskofu,katika Kanisa la Bukoba

Misa takatifu ya Kumsimika Askofu Rwoma kuliongoza Jimbo la Bukoba


April 6&7, 2013 imekuwa zimekuwa siku za Kumbukumbu na kihistoria katika Mkoa wa Kagera hasa kwa wafuasi wa dini ya Kikristo wa dhehebu la Katoliki. Historia hiyo ni kutokana na Ibaada ya Kumsimika Askofu wa jimbo Katoliki la Bukoba Mhashamu Desderius Rwoma.

Shughuli hiyo imewakutanisha Viongozi mbali mbali wa kidini, wakiwemo Balozi wa Papa nchini Tanzania Askofu mkuu Francisco Pardira , maaskofu wakuu,maaskofu,Mapadre,watawa na walei,lakini pia viongozi wa serikali,Mashirika na Vyama vya siasa.  Na chini kwa chini unaye msikia ni Mhashamu Baba askofu Severin Niwemugizi wa Jimbo katoliki la Rulenge Ngara ambaye ni makam Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania akitamburisha wageni wa sherehe hizo
Katika maadhimisho ya misa Takatifu yaliyofanyika katika Kanisa Kuu la Jimbo la Bukoba,Viongozi wa Dini na wa serikali walipata fursa ya kutoa ujumbe kwa waumini na wananchi waliohudhuria katika sherehe hizo
Wa kwanza kuzungumza na umati mkubwa wa watu waliohudhuria alikuwa askofu mstaafu  wa jimbo hilo Nestory Timanywa,ambaye kwa kiasu kikubwa alitumia muda wake kuwashukuru waumini kwa ushirikiano mkubwa wakati wa uongozi wake

Balozi wa Papa hapa Nchini,Askofu mkuu Francisco Pardira amewataka waumini kumuombea Askofu Rwoma ili aweze kuitenda kazi ya bwana kwa mafanikio
 Aidha, katika sherehe hizo, Rais mstaafu wa awamu ya tatu hapa nchini  Benjamin William Mkapa alipewa nafasi ya kuzungumza na akamtaja askofu Desderius Rwoma ambaye amehamia Bukoba akitoka Jimbo Katoliki la Singida kuwa amekuwa msaada mkubwa uliomuwezesha kuliongoza kwa mafanikio  Taifa kwa miaka kumi
Askofu Rwoma, licha ya kuhamia Bukoba ataendelea kuwa msimamizi wa kitume jhimbo la Singida ambalo ameliongoza kwa miaka 14 hivi sasa
Askofu huyo alizaliwa May 08 1947 katika kijiji cha Ilogero Parokia ya Rutabo. Nikiripoti kutoka Bukoba

No comments:

Post a Comment