April 12, 2013

Mbasa ahoji wananchi kudaiwa kuishi hifadhini

JIBU LA SWALI LA MBUNGE Biharamulo magharibi
MBUNGE wa Biharamulo Magharibi, Dk. Antony Mbasa (CHADEMA) ameihoji serikali ni kwanini imedai kuwa wananchi wanaoishi katika maeneo ya Mania na Miango katika wilaya hiyo wanadaiwa kuishi katika hifadhi ya wanyama.
“Nataka kuelewa ni kwanini serikali inadai kuwa wakazi wa Kania na Miango wanadaiwa kuishi katika hifadhi ya wanyama wakati zaidi ya miaka 50 iliyopita watu walikuwa wakiishi hapo ambapo hata Profesa Kulikoyela Kahigi alizaliwa,” alihoji Dk. Mabasa wakati akiuliza swali la nyongeza bungeni jana.
Awali katika swali la msingi, Mbunge wa Liwale, Feith Mitambo (CCM) alitaka kujua serikali itamaliza lini mgogoro wa mpaka kati ya Kijiji cha Kikulyangu na pori la akiba la Selous ambao umedumu zaidi ya miaka 10.
Aidha alitaka kuelezwa ni lini serikali itahakiki mpaka huo kama ulivyo kwenye tangazo la serikali la mwaka 1974.
Akijibu swali hilo, Naibu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Lazalo Nyalandu alisema mgogoro huo unashughulikiwa na wizara yake tangu mwaka 2010 kwa kushirikiana na Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Alieleza Halmashauri ya Wilaya ya Liwale na Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya MAGINGO wanaendelea kushughulikia tatizo hilo.
Alisema mwaka 2010 wizara ilihakiki mpaka kati ya pori la akiba la Selous na vijiji vinavyounda WMA ya Liwale kwa kuzingatia maelezo ya tangazo la serikali namba 275 la mwaka 1974.

  Habari kutoka Bungeni Dodoma. source Tanzania Daima

No comments:

Post a Comment