October 15, 2013

RAIS KIKWETE AZUNGUMZA NA VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA IKULU -DAR ES SALAAM

Makundi ya wanaharakati nchini huenda wakakutana na Rais Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar Es Salaam kati ya kesho au keshokutwa, kwa ajili ya mazungumzo kuhusu Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba


Hatua hiyo inakuja baada ya Rais Kikwete kukutana na kundi la viongozi wa vyama vya siasa vyenye uwakilishi Bungeni na kujadili mambo mbalimbali kuhusu marekebisho ya Muswada huo.

Rais Kikwete leo amekutana na viongozi wa CUF, Chadema na NCCR-Mageuzi na kujadiliana kasoro kadhaa zilizopo kwenye Muswada huo uliozua utata na kusababisha vyama hivyo kuitisha maandamano ya nchi nzima kupinga musawada huo usisainiwe na rais kabla ya kuyasitisha maandamano hayo

Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba nchini (Jukata) Bw Deus Kibamba, amesema kuwa wameahidiwa kuwa wanaweza kuonana na Rais kati ya Jumatano au Alhamisi kwa ajili ya kujadili Muswada huo

No comments:

Post a Comment