November 17, 2013

Profesa Tibaijuka Awaonya Madiwani ccm kuacha Malumbano ya Kisiasa




MULEBA:
Madiwani na viongozi wa CCM wilayani Muleba mkoani kagera  wametakiwa kuacha malumbano ya kisiasa na badala yake  yake wahimize upatikanaji wa maendeleo kwa wananchi

Waziri wa Ardhi na maendeleo ya makazi Profesa Anna Tibaijuka ametoa kauli hiyo jana kwenye kikao cha madiwani wa ccm na viongozi wa chama hicho  katika kuondoa migogoro iliyopo kwa viongozi hao wilayani humo

Profesa Tibaikuka maesema kuwa vitendo vya kulumbana na kuendeleza migogoro ni kukiweka chama katika mazingira magumu katika uchaguzi ujao na wanachi kushindwa kuamini wakiwemo viongozi waliowachagua

Prof Tibaijuka akisaini kitabu cha wageni,pembeni yake ni m/kiti wa CCM  wilayani Muleba Muhaji Bushako

Profesa Anna Tibaijuka akisaini kitabu katika kufanya mkutano na viongozi wa ccm wilayani Mulena kulia ni Mwenyekiti wa CCM wilayani Muleba Muhaji Bushako

Hata hivyo Mwenye kiti wa CCM wilayani Muleba Bw Muhaji Bushako amesema malumbano yalisababishwa na ukiukaji wa misingi ya uongozi na katiba ya chama lakini  sasa kuna maridhiano na migogoro sasa imekwisha.

Vijana washauriwa kuwa wajasiliamali
Na Shaaban Ndyamukama November 12, 2013
MULEBA
Waziri wa ardhi na maendeleo ya makazi profesa Anna Tibaijuka amelitaka kundi la Vijana kujiunga katika vikundi vya uzalishaji mali na kufanya kazi kwa juhudi na maarifa ili kujiletea maendeleo kwenye maeneo yao

Profesa Tibaijuka ametoa wito huo jana katika ziara yake ya kutembelea wnanchi wa kijiji cha kisana wilayani Muleba katika kukagua miradi ya maendeleo na kwamba vikundi vyenye miradi ataviwezesha kiujasiliamali

Amesema kundi la vijana lina maisha ya kutegemea ajiraa kutoka serikalini lakini fursa hiyo inapatikana kw watu wachache tena wenye taaluma  ambao ni katika nyanja za elimu afya na miundombinu

Hata hivyo Profesa Tibaijuka jana ametoa Jumla ya shilingi milioni 1.3 kwa ajili ya kuwezesha vikundi vya ujasiliamali vya kata ya  Kyebitembe  kikiwemo cha vijana cha kutokomeza ugonjwa wa mnyauko wa migomba.


Wananchi waomba kuongezewa nguvu za ujenzi wa zahanati ya kijiji
Na Shaaban Ndyamukama November 12, 2013
MULEBA
Wananchi wa kijiji cha kisana wilayani Mulea mkoani Kagera wamejenga zahanati yao ya kijiji  kwa kukusanya vifaa vinavyopatikana katika maingira yao ambavyo thamani yake ni shilingi milioni 17.8 bila nguvu za serikali

Diwani wa kata ya Kyebitembe wilayani Muleba Bw Vedasto Rwechungura amesema hayo jana wakati akitoa taarifa ya maendeleo kwa  waziri wa ardhi na mendeleo ya makazi Profesa Anna Tibaijuka

Bw Rwechungura amesema zahanati hiyo jengolake limefikia hatua ya kufunga linta ambapo kijji hicho kilijenga baada ya kutenga maeneo ya huduma za jamii katika matumizi bora ya ardhi


Waziri Tibaijuka akikagua jengo la zahanati la kijiji cha kisana wilayani Muleba linalojengwa kwa Nguvu za wananchi jinsi linavyoonekana ,mwenye skafu ni diwani kata ya Kyebtembe Vedastus Rwechungura
 
Mkurugenzi mtendaji wa H/w ya MulebaBi Oliva Vavunge akifafanua kuhusu ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Kisana
Hata vivyo Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Muleba Bi Oliva Vavunge amesema mwaka huu zimetengwa shilingi milioni 60 kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa zahanati hiyo ili kuwapa nguvu wananchi kujitolea.




WORLD VISSION yasaidia jamii  Kujenga  vyumba vya madarasa
 Na Shaaban Ndyamukama

MULEBA
Shirika la world vision kanda ya kagera jana limekabidhi vyumba vitatu vya madarasa katika shule ya msingi Nyailigamba wilayani Muleba mkoni Kagera vilivyojengwa kwa Tsh.mil 36.7 zikiwemo Nguvu za wananchi

Diwani wa kata ya Muhutwe Magongo Justus amesema ujenzi huo umefanyika kunusuru wanafunzi 400 wa shule hiyo kujifunzia mazingira magumu ikiwa nguvu za jamii ni Tsh.mil 2.4 na mbunge wa Muleba kaskazini amechangia matofali 30,000

Justus amesema kuwa halmashauri ya wilaya ya Muleba imechangia Tsh Mil 6 na mkuu wa wilaya hiyo Lambris Kipuyo alichangia Tsh 600,000/-  na kwamba vyumba hivyo vitatumika kwa alengo yaliyokusudiwa

Hata hivyo Meneja wa world vision Kanda ya kagera Misigaro Mpiti amesema shirika lake linasaidia jamii changamoto zilizoibuliwa na kupewa kipaumbele katika kuhitaji misaada




No comments:

Post a Comment