Mh.Conchester Lwamulaza akizungumza na Wanawake Wilayani Biharamulo |
Na Juventus Juvenary-BIHARAMULO
Mwenyekiti wa Baraza la wananwake
Chama cha Demokrasia na Maendeleo BAWACHA na Mbunge wa viti maalum mkoani Kagera Bi.Conchester Lwamulaza amewataka
wanawake mkoani humo kuhakikisha kuwa wanajiandikisha katika daftari la kudumu
la wapiga kura na kuytumia haki yao kikatiba kugombea nafasi mbali mbali za
uongozi katika serikali za mitaa
Bi.Lwamulaza ametoa wito huo July
14, mwaka huu wakati akizungumza na vikundi vya wanawake katika ziara ya Mbunge
wa jimbo la Biharamulo Magharibi Dk.Anthony Mbassa ya kutembelea vikundi hivyo
Mbunge huyo
amesema sasa ni wakati wa wanawake kutumia fursa hiyo ya uchaguzi wa
serikali za mitaa kujitokeza kugombea nyadhifa mbalimbali za kuongoza katika
ngazi ya vijiji na vitongoji
Aidha,Bi.
Lwamulaza amesema mbali na kujiandikisha katika daftari la wapiga kura,wanawake
hao pia wanatakiwa kutunza shahada zao ili kuepuka kudanganywa na wajanja
kwakununua kadi zao ili kuwakwamisha kushiriki katika uchaguzi.
Mbunge wa Jimbo la Biharamulo Magharibi Dk.Anthony Mbassa
amewataka wananchi jimboni humo kutumia
ufugaji wa nyuki kama chanzo rahisi cha mapato na njia mbadala ya
utunzaji wa mazingira
Dk.Mbassa amesema hayo wakati wa ziara yake ya kutembelea na
kukagua miradi inayoendeshwa na vikundi vya wanawake ndani ya jimbo hilo
Akizungumza na wanawake wa kata za Nyabusozi,Runazi na kabindi
katika Vikundi vya Nyabusozi,Kiluhula,Mubaga,Nyamazike na
Aidha,amesema ufugaji wa nyuki ni rafiki wa mazingira kwakuwa
wafugaji wanakuwa makini kuchunga mizitu isiungue moto ili kuepuka hasara ya
kupoteza mizinga.
Na katika utunzaji wa Mazingira!!
Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Kabindi Wilayani Biharamulo
Mkoani Kagera wameilalamikia halmashauri ya Wilaya hiyo kukusanya mapato
kutokana na ushuru wa Soko bila kurekebisha miundombinu
Wananchi hao wamesema hayo wakati wakizungumza na Mbunge wa jimbo la Biharamulo Magharibi
Dk.Anthony Mbassa katika ziara ya kutembea na kukagua shughuli za maendeleo ya
Vikundi vya Wanawake katika kata hiyo
Mmoja wa wananchi hao Bw. Dismas Mathew amesema kutokana na mapato Halmashauri inayokusanya
kutokana na ushuru huo hainabudi kuyatumia katika kurekebisha miundombinu
sokoni hapo kwa kujenga chanja za kupangia bidhaa
Radio Kwizera Fm imeshuhudia baadhi ya bidhaa za vyakula
kama Viazi na mihogo vikipangwa chini
jambo ambalo kiafya ni hatari
Kutokana na hali hiyo Mbunge wa jimbo la Biharamulo Magharibi
Dk.Anthony Mbassa amemwagiza Diwani wa kata ya Kabindi Bw.Benezett Muhoza
kulifikisha katika vikao vya maendeleo
ya kata ili lijadiliwe na kutafutiwa ufumbuzi.
Mbali na uzinduzi pamoja na ukaguzi huo,wabunge hao pia walitoa zawadi mbali mbali ikiwa ni pamoja na Kikundi cha Nyakahura kukabidhiwa Baiskeli
No comments:
Post a Comment