August 17, 2014

Magufuli: Sina mpango wa urais


Source:Tanzania daima.
WAZIRI wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, amesema kuwa hana mpango na urais wala kujitangaza kuwania nafasi hiyo.
Hatua hiyo ilitokana na wananchi wengi kumshangilia na kumwita rais wakati ziara ya siku tatu ya kukagua miradi ya ujenzi wa barabara, madaraja na vivuko.
Akiwa katika eneo la Tegeta, aliwaeleza wananchi kazi ambazo serikali imekuwa ikizifanya katika kuhakikisha inaondoa adha ya foleni jijini Dar es Salaam ambapo wakimshangilia na kumpatia sifa za kuwa rais 2015.
Hata hivyo, Dk. Magufuli alikanausha habari hizo na kueleza kuwa ni maono ya wananchi na si yeye.
“Sina mpango huo nipo katika ziara kuangalia utendaji wa watu tuliowapatia kazi, hayo ni maono yao,”alisema.
Magufuli anaonekana kuwa tofauti na baadhi ya vigogo wa CCM ambao kwa nyakati tofauti wamekuwa wakijinadi kuusaka urais.

No comments:

Post a Comment