March 3, 2013

KILIMO NA MIFUGO NDIO MKOMBOZI WETU



Hii ndio Ngara. na watu wa kuoikomboa Ngara ni mimi na wewe!



Siku ya leo ngarakwetoblog imekutana uso kwa uso na mtaalam wa Kilimo na Mifugo Jonas Kizima. Kwa asili ni mzaliwa wa Kijiji cha Buhororo Ngara, kwa sasa yuko Chuo kikuu cha Sokoine Morogoro, ambaye katika safu hii anakuja na somo:-




 ___________________________________________________




Sekta ya mifugo kama zilivyo shghuli nyingine za kibinadamu za uzalishaji mali za, ni miongoni mwa sekta zenye kuhusika katika uharibifu wa mazingira kama shughuli hizo hazijawekewa mikakati na jamii au mamlaka husika.  Lakini pia mbali na uharibifu wa mazingira pia sekta ya mifugo pamoja na watumiaji wengine ardhi  huweza kusababisha  migongano ya matumizi ya rasilimali

 

 Mifugo imekuwa ikinyooshewa vidole na sekta nyingine Mfano mamlaka za barabara kuharibu kingo za barabara. Kwani mfumo wetu wa ufugaji haujaweza kutengenisha au kuainisha rasmi mgawanyo au mpango wa matumizi bora ya ardh ili kila sekta iweze kuwa na mifumo yake ili KUEPUSHA MIGGOGORO , kutokana na uharibifu wa mali au uvunjifu wa amani katika jamii


Katika Picha. Mtaalam(Mtafiti) Jonas B.Kizima kutoka Chuo Kikuu Sokoine akipima nyasi kwa kipimo maalumu. ni katika Jitihada za kuboresha marisho ya Mifugo
  

            Katika picha hapo juu linaonekana kundi la Ng'ombe wakipelekwa malishoni
Taswira ya Rusumo

Baadhi ya maeneo ya Rusumo kwenye vilima/miteremko yanayoonesha dalili za uharibifu wa mazingira unaoweza kuleteteleza mmomonyoko wa ardhi kutokana na mifugo kuyatumia maeneo ya malisho kupita kiasi. Bado upo umuhimu wa wataaalamu kupima na kuainisha uwezo wa eneo la malisho kujua ni mifugo mingapi inaweza kulishwa eneo hilo, ili kutoa ushauri kwa wafygaji  na wadau wengine ili kuongeza uzalishaji wa mazao ya mifugo na kuepusha uharibifu wa nyanda za malisho ( overgrazing)
 
Timu ya wataalam ikipata maelezo kutoka kwa meneja wa REDESO Ngara Bw. Leonce Batondana
 Jitihada mbalimbali za mashirika zimekuwepo wilayani Ngara kusaidia kuhifadhi mazingira na vyanzo vya maji, hapa mtaaalamu ( Meneja wa shirika la REDESO ndugu Leons BATONDANA akitoa maelezo kwa wageni kuhusu jitihada za shirika lake kwa kusaidiana na mashirika mengine kuzalisha miche ya MITI ya ASILI ipatikanayo kweneye vyanzo vya maji ili iweze kupandwa katika vyanzo vya maji ( water catchment

Kulia katika Picha ni Ndg. Leonce Batondana, Meneja wa mradi REDESO  akitoa maelezo katika moja ya vitalu vya kuoteshea miche ya miti
 


Shamba darasa
  
Kilimo Mseto


Shamba linapendeza
www. ngarakwetu.blogspot inapenda kukushukuru ndugu Jonas B. Kizima, mtaalam wa mifugo na Kilimo. tunatambua mchango wako na tunaamini kwa jitihada zako sekta ya mifugo na kilimo itawanufaisha wananchi wa Ngara na kuwakwamua Kimaisha. nasi tunaahidi ushirikiano mkubwa katika kuhakikisha dhamira ya dhati ya maendeleo inatimilizika

No comments:

Post a Comment