October 23, 2012

Wasimamizi wa mtihani wa Form IV wilayani Ngara watakiwa kuwa na uadilifu

Baadhi ya walimu wakipata semina elekezi ya usimamizi wa mitihani


Na Shaaban Ndyamukama Ngara
Wasimamizi wa mtihani wa kuhitimu kidato cha nne katika wilaya ya Ngara mkoani Kagera wametakiwa kufanya kazi waliyopewa kwa umakini na kutumia uadilifu kwa lengo la kuleta ufaulu wenye sifa kwa wanafunzi watakaochaguliwa kuendelea na masomo ya juu
Mkuu wa wilaya ya Ngara Bw Costantini Kanyasu alisema hayo Oktoba 6 wilayani Ngara katika ukumbi wa Ngara sekondari kwenye  semina ya mafunzo elekezi kwa wasimamizi 135 walioteuliwa kusimamia mtihani wa kidato cha nne ulioanza oktoba 8 kote nchini
Kanyasu alisema kuwa wasimamizi hao wajiepushe na udanganyifu wa mitihani wa kusaidia wanafuzi wasiojiweza kitaaluma na hatimaye kupata wataalamu na watumishi wa kada mbalimbali wasiojiweza katika kutoa huduma kwa taifa
Alimtaka kila msimamizi kuwajibika kwa kufuata maelekezo na mwongozo wa baraza la mitihani la taifa na kuandaa vijana watakao kuwa na manufaa ndani ya jamii kwa kuzingatia kanuni taratibu na sheria  kuliko kuwa na vijana waliokwenda shule lakini wanakuwa wategemezi wa taifa na kuendelea kuwa maskini kwa kukosa uadilifu
Naye Afisa elimu sekondari wilayani Ngara Bw Julias Nestory alisema katika mtihani huo wilaya ya Ngara itakuwa na watahiniwa 2471 kati yao 141 ni wale wa kujitegemea na kutakuwa na vituo28 na kila chumba cha mtihani hakitazidisha wanafunzi 40.Nestory alisema vijana wa kike baadhi yao wamejifungua na hawataruhusiwa kufanya mtihani wa taifa wa kuhitimu elimu ya sekondari na wale wa kiume wamekimbia familia zao kwa kukosa mahitaji muhimu ya elimu na kwenda kuwa vibarua katika mikoa jirani  kwenye mashamba ya miwa na tumbaku.  Alisema kuwa jamii haina budi kuwamakini katika kuwekeza kwenye elimu kwani kati ya wanafunzi 2844 waliosajiliwa kidato cha kwanza wilayani Ngara wanafuzi 543 hawatafanya mtihani huo kutokana na sababu mbalimbali zikiweo za wazazi kushindwa kutoa mahitaji kwa watoto wao
Mara baada ya kuanza mtihani huo  siku ya jumatatu oktoba 8 mwanafunzi wa shule ya sekondari Muyenzi wilayani Ngara Alexander Victor miaka 18 aliugua ghafla katika shule hiyo baada ya kumaliza kipindi cha kwanza cha somo la Civics
Kwa mujibu wa mkuu wa shule ya sekondari Muyenzi Dickson Mwombeki (Mwenye koti Jeusi Pichani ) alisema mwanafunzi huyo alipelekwa katika Hospitali ya Misheni Rulenge  kwa msaada wa gari la  Afisa Elimu sekondari wilayani Ngara Juliu Nestory  Kilomita saba toka shuleni hapo na kulazwa kabla ya kufanya somo la English. Akiongea na mwandishi wa habari hizi mdogo wake na Mwanafunzi huyo Nelson Victor anayesoma kidato cha pili shuleni hapo alisema kaka yake alikuwa mgonjwa siku tatu kabla ya mtihani akisumbuliwa na homa kuumia miguu wakati wa kutembea pamoja kushindwa kula
Kwa upande wake Mganga mkuu wa Hospitali ya Rulenge Dr Magnus Banyikila alisema mwanafunzi Alexander aliugua ghafla kwa kupata maumivu ya mwili na kichwa na amepata matibabu na kwa sasa ameruhusiwa kuendelea na masomo yanayofuata kwa mujibu wa ratiba ya mtihani huo wa taifa
Afisa elimu sekondari wilayani Ngara Juliu Nestory alithibitisha taarifa za kuugua mwanafunzi huyo na kwamba kiafya amerudi katika hali yake ya kawaida na kuungana na wenzake kufanya mtihani na somo ambalo hakulifanya taarifa za daktari zitakuwa ni ushahidi kuondoa malalamiko

No comments:

Post a Comment