July 13, 2013

UPADIRISHO-JIMBO KATOLIKI LA RULENGE NGARA

Mhashamu Baba Akofu Severin Niwemugizi wa jimbo Katoli la Rulenge Ngara akingia katika Kanisa la Mt. Francisco parokia ya Biharamulo kutoa daraja la Upadre kwa Shemasi Fortunatus Rweikiza

Akimuombea kabla ya kumpadirisha

Shemasi Fortunatus Rweikiza muda mfupi kabla ya kupadirishwa

Askofu Niwemugizi akimwekea mikono kwaajili ya Baraka

Mbele ya Shemasi Rweikiza muda mfupi kabla ya Kupadirishwa, Mapadre walimuombea. Anayeonekana hapo ni Padre Damas Missanga ambaye i Mkurugenzi wa Radio Kwizera

Hapa ni baada ya kupadirishwa na kuvalishwa rasmi Mavasi ya Upadre

baada ya Kupewa daraja la Upadre akaombea ili kuitenda kazi ya utume

Askofu Niwemugizi akimpaka mafuta ya Krisma



Askofu wa jimbo jilo Mhashamu severini Niwemugizi,Ijumaa ya Julai 12,mwaka huu ametoa Daraja la Upadre kwa aliyekuwa shemasi Fortunatus Rweikiza. Misa takatifu ya Upadirisho kwa Padre Fortunatus imefanyika katika Kanisa Katoliki la Mt. Francisco parokia ya Biharamulo.


Aidha katika hatua nyingine Askofu Niwemugizi ametoa wito kwa waumini wa Kanisa hilo kujenga tabia ya kufunga ndoa na kuachana na dhana visingizio vya gharama kwaajili ya harusi, na kuwataka wazazi kuhimiza watoto wao kufunga ndoa na kukemea vikali visingizo vya mahari kwakuwa mambo hayo hayana uhusiano na Kanisa


No comments:

Post a Comment