July 11, 2014

RC KAGERA ASISITIZA HAKI ZA WAZEE KUMILIKI ARDHI

Picha kutoka maktaba: Kulia mwenye kibaragashia kichwani(Juventus Juvenary) nikiwa na mzee Jovin Barahemana,Jovitho Jovin na wakazi wa Kijiji cha Mayenzi kata ya kibimba tukijadili masuala ya Ardhi
Mkuu wa mkoa wa kagera kanal Fabian Massawe amewataka wazee wenye malalamiko ya kuporwa ardhi na watu wenye uwezo kifedha kupeleka malalamiko yao Serikalini ili wahusika wachukue hatua na wazee wapate haki yao ya kumiliki Ardhi
Kanal Massawe amesema hayo kutokana na malalamiko ya baadhi ya wazee  wilayani Biharamulo Mkoani Kagera kuomba serikali kuweka utaratibu maalum wa kushughulikia migogoro ya ardhi inayowakabili wazee hao kwa madai kuwa wananyanyaswa na watu wenye uwezo kifedha wanaovamia na kujimilikisha maeneo yao
Wakizungumza na Radio Kwizera kwa nyakati tofauti wilayani humo,Wazee hao wamesema kutokana na matendo hayo wamejikuta katika hali ngumu kwakuwa hawana mtetezi
Mmoja wa wazee hao  Domician Rwelamura mkazi wa kijiji cha Lukora kata ya Runazi amesema kuwa zaidi ya hekari 3 za shamba lake zimevamiwa na mtu mmoja ambaye hata hivyo amefanya naye kesi mahakamani kwa zaidi ya miaka 2 na bado haki haijapatikana

Kutokana na Malalamiko hayo Mkuu wa Mkoa wa Kagera Kanal Fabiani Massawe ameziagiza mamlaka husika kuhakikisha wanatumia vizuri nafasi zao kutatua migogoro hiyo na kuwachukulia hatua watu wanaotumia uwezo wao kifedha kupora ardhi na kuwanyima haki wazee.     EndS


Mzee Domician Rwelamura,mkazi wa Lukora Biharamulo akizungumza nami namna alivyoporwa ardhi na kigogo mwenye pesa

Akionesha nyaraka na vielelezo

No comments:

Post a Comment