July 13, 2014

UJERUMANI MABINGWA KOMBE LA DUNIA 2014

hatimae mchaka mchaka wa takribani mwezi mmoja wa michuano ya kombe la dunia umefika tamati nchini Brazil ambapo mechi ya fainali iliyoikutanisha miamba miwili ya Soka Ujerumani vs Argentina jijini Rio de Janeiro kwenye uwanja wa Maracana kumalizika huku Ujerumani wakiibuka mabingwa.
Ushindi ni wa Ujerumani wa goli moja tu lililofungwa ndani ya dakika 30 za nyongeza baada ya full time kuwa 0-0 na mfungaji  Mario Gotze aliesababisha Ujerumani kuchukua ubingwa wake wa nne wa dunia.
Tuzo ya mchezaji bora wa mashindano imeenda kwa Lionel Messi, mfungaji bora James Rodriguez, kipa bora Manuel Neur na mwanasoka bora chipukizi wa mashindano amechukua Paul Pogba.

No comments:

Post a Comment